NA CHAUSIKU SAID _MWANZA.
Jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza linawashikilia watu watano kwa tuhuma za kuhusika na mauji ya watu watatu wa familia moja kwa kuwakatakata na mapanga.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza Ramadhani Ng'anzi amethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao waliofanya mauaji hayo mnamo tarehe 18 mwezi huu majira ya saa 5 usiku eneo la Mecco kusini wilaya ya Ilemela.
Ng'anzi ameeleza kuwa baada ya jeshi la polisi kupata taarifa za mauji hayo walianza upelelezi wa kina na kuweza kuwakamata watuhumiwa hao watano huku wakiwa na vielelezo mbalimbali ikiwemo mali za marehemu walizopora baada ya tukio.
Amesema kuwa baada ya upelelezi jeshi la polisi limegundua chanzo cha mauji hayo ni mgogoro wa kibiashara kati ya marehemu na Watuhumiwa
Ameeleza kuwa baadhi ya vitu walivyopora kwa marehemu ni pamoja na fridge aina ya kyoto, godoro moja lenye ukubwa wa futi 4 kwa6, Tv mbili aina ya singsung zote inchi 18, Radio mbili (2) moja aina ya seapiano, jiko moja la gesi aina ya nikle pamoja na simu tatu (3) aina ya tecno zilizopatikana nyumbani kwa mmoja wa mtuhumiwa maeneo ya buhongwa.
Ng'anzi ameeleza kuwa baada ya mahojiano watuhumiwa wamekiri kutenda matukio hayo huku wakiwa na silaha aina ya panga lililotumika kutendea tukio hilo.
Amewataja watuhumiwa waliohusika na mauaji hao ni pamoja na Thomas Jilala mwenyewe umri (26) msukuma mkokoteni mkazi wa Buhongwa, Hajir Thomas mwwenye umri(23) fundi cherehani mkazi wa buhongwa , Deoglas Vicent mwenye umri (31) Emmanuel Charles mwenye umri (36) Operator wa mitambo katika mgodi wa Mwadui mkazi wa mecco kusini.
Hata hivyo ameeleza kuwa watuhumiwa watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi wa tukio hilo kukamilika na hatua za kisheria kuchukuliwa.
Aidha ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi kuhakikisha wanatokomeza vitendo vya uhalifu na kutoa onyo kwa wale wote wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu na kujichukulia sheria za mkononi hawataweza kukwepa mkono wa sheria.
0 Comments