Header Ads Widget

WATOTO WANNE WA FAMILIA MOJA WAPIGWA NA RADI KIGOMA NA KUFARIKI DUNIA

 




WATOTO wanne wa familia moja wamefariki dunia baada ya kujeruhiwa na radi kufuatia mvua kubwa iliyonyesha ambayo iliambatana na radi.........Na Editha Karlo,Kigoma


Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya tukio hilo kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kigoma James Manyama alisema kuwa tukio hilo limetokea tarehe 4 mwezi huu majira ya saa 12 jioni katika kijiji cha Kibuye kata ya Kumsenga,Tarafa ya Mabamba Wilaya ya Kibondo.


Kamanda aliwataja marehemu hao kuwa ni Baseka Japhet(10)mwanafunzi wa darasa la tano,Goma Jeremia(5),Rock Ramadhani(5)Alam Pascari(9)Annatoria Muhoza(50)Mkulima mkazi wa kijiji cha Kibuye.


Kamanda alisema watoto hao wanne wakati mvua inaendelea kunyesha  walikuwa wakicheza chini ya mti wa mwembe nje ya nyumbani kwao ndipo walipopigea na radi na kupelekea vifo vyao.


Aidha katika tukio hilo marehemu aitwaye Annatoria Muhoza(50)yeye alipigwa na radi wakati akiwa shambani akiendelea na shughuli zake za kilimo.


Miili ya marehemu wote imehifadhiwa hospital ya Wilaya ya Kibondo kwaajili ya uchunguzi zaidi,Kamanda ametoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Kigoma hasa katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha kujikinga mvua ndani ya makazi yao wanamoishi waepuke kujikinga mvua chini ya miti.


"Niwasihi wazazi na walezi wote kuwaangalia watoto wao kwa ukaribu hususani kipindi hiki cha mvua zinazoendekea kunyesha,kuwazuia watoto wao pia wasicheze nje wakati mvua inanyesha"alisema Kamanda Manyama

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI