Header Ads Widget

ASKOFU BAGONZA :MWISHO WA NGUVU, MWANZO WA HEKIMA

Mkuu wa nchi ameongea tayari. Tumeona sura mpya tofauti na ile tuliyoizoea. Ukimgeuza sana nyoka utaona miguu yake. Yanasemwa mengi na wengi. Mimi nina mawili:


1. Ni nafasi ya Mama kuanza upya. Mvutano wa mihimili unafaa kama ni wa vyama tofauti. Ni hekima kumpa nafasi Mama bila kusubiri kuombwa kupisha. Ni salama na heshima kupisha ukarejeshwa kuliko  kuambiwa umpishe mgeni akae.


2. Mke wa Kaizari anapaswa kuishi nje na ng'ambo ya tuhuma ya uzinzi.Tuhuma zinatosha kuvunja ndoa yake. Wanaotuhumiwa na Mama kuota 2025 wampishe bila kusubiri mkeka. Akipenda atawarejesha mwenyewe. Hiyo ni busara, siyo nguvu.


Arobaini za swala zikifika, huwa hasikii baragumu ya wawindaji.

Shtuka bila kuchelewa.

 Na Askofu Benson Lwakalinda Bagonza ameandika



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI