Wananchi mkoani Kilimanjaro wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika maktaba ya mkoa ili kujisomea vitabu mbalimbali vilivyopo na waweze kujipatia maarifa yaaliyopo kataka vitabu hivyo........Na, Rehema Abraham
Wito huo umetolewa Mkutubi wa maktaba ya Mkoa ya Kilimanjaro Enoky Mwangombe wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Ofisi ya maktaba hiyo iliyopo Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Amesema kuwa ni vyema wananchi wakahudhuria kujisomea vitabu katika maktaba hiyo kwani inatoa huduma kwa watu wote ,kama wanafunzi,wananchi wa kawaida wafanyabiashara na hata wakulima.
Sambamba na hayo amesema kuwa changamoto iliyopo katika maktaba hiyo ni baadhi ya wasomaji wanaofika katika maktaba hiyo kukosa baadhi ya vitabu , wanavyovitaji kijisomea .
Amesema kuwa kila mwezi kunakiwepo jarida la mkulima (mkulima mbunifu) ambao wakulima wamekuwa wakijisomea na kuweza kuwasaidia katika kuboreshea shughuli za kilimo ,na pia kwa wafanyabiashara vitabu vya biashara vinakuwepo ambavyo wakijisomea wanapata uelewa wa kukuza biashara zoa.
Hata hivyo Amesema kuwa maktaba hiyo ipo katika utaratibu wa kulibadilisha mfumo wa usomaji kuwa katika mfumo wa kidigitali ili kiendana na wakati uliopo
1 Comments
Congratulations keep it up
ReplyDelete