Serikali wilaya ya Kilosa mkoa Morogoro kwa kushirikiana na Viongozi wa Dini na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya humo wameanza upya zoezi la kutoa elimu kuhusu faida za Chanjo ya UVICO 19 baada ya takwimu za hali uchanjaji kutoridhisha katika wilaya hiyo
Mganga Mkuu wa wilaya ya Kilosa Dokta George Kasimbate anasema Wilaya hiyo ina zaidi ya wakazi laki Tano (500,000)huku matarajio kuchanja watu laki tatu na ishirini elfu (320,000 )lakini hadi sasa waliochanja ni watu elfu ishirini na nne tuu (24,911) jambo ambalo hairdthishi
Dokta Kasimbante anasema mpango wa Serikali ni kufikia asilimia sitini kwa watu waliochanja hivyo wameona ni vyema kushirikisha viongozi wa dini ,na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi ambao wanaushawishi mkubwa katika jamiii
Anasema wamebaini bado wanachi wengi vijijini hawafahamu elimu kuhusu faidi za chanjo ya UVICO 19 hivyo elimu inayotolewa italeta manufaa katika zoezi hilo
Kwa upande wake Shekh Mkuu wilaya ya Kilosa Alhaj Nassoro Milambo anasema wapo baadhi ya watu wanakataa kuchanja Kwa kisingizio Cha Imani za kidini hivyo wanaendela kuwaelimisha waumini wao kuwa suala la afya ni muhimu hata vitabu vya dini vimeelekeza.
Shekh Milambo anaongeza Kwa kusema vitabu vya dini vimeelekeza tuheshimu mamlaka zilizopo duniani kwani zimewekwa na mungu hivyo Viongozi wa Serikali hawawezi kuleta chanjo zenye madhara kwa wananchi wake wanaachi wasiogipe kuchanja
Naye katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kilosa Shabani Mdoe anasema kitendo Cha Rais Samia Suluhu Hassan kuruhusu chanjo ametimiza ilani ya uchaguzi ya Chama hicho kwani imelekeza Serikali kujali afya za wananchi huku Mkuu wa wilaya hiyo Alhaj Majd Mwanga akisisitiza suala la wananchi kujiandaa na Sensa ya watu na makazi inayotarajia kufanyika mwezi agost mwaka huu 2022 na kwamba hiyo itakua dira ya Serikali kutenga bajeti kubwa katika sekta ya Afya kulingana na unitaji .
0 Comments