Header Ads Widget

MBUNGE ATAKA UFUMBUZI WA MPAKA WA TARAFA

                       mbunge Kimei

Mbunge wa korogwe mjini Mh Alfred Kimea ametaka mgogoro wa mda mrefu wa wapi Tarafa  ya  magoma inatakiwa iwepo kiutawala utatuliwe Mara moja   ili kusogeza huduma karibu na jamii.  Mwandishi Ibrahim Kunoga Tanga


Kauli hiyo ameitoa katika kikao cha kamati ya ushauri wa mkoa RCC


Tarafa hiyo aijulikani kama ipo  korogwe mji au kijijini jambo ambalo hata wakati wa uchaguzi limekuwa likiibuka kwa siasa ambazo kila mgombea wa majimbo hayo mawili amekuwa akiamini eneo hilo ni lake.

Mh kimea alisema maendeleo yoyote lazima yawepo kati ya wachaguliwa na wale wanaochagua kwa hiyo magoma imekuwa kama imetengwa hivyo yeye kama mbunge ambae anahitaji kurudi kwa awamu ya pili natakiwa niwe karibu na watu wangu kuhakikisha wanapata maendeleo kwa wakati ili waweze kunichagua kwa kipindi cha awamu ya pili 

"Ngugu yangu Mzava ni mbunge wa korogwe vijijini kama magoma itakuwa imerudi mjini hatakuwa na majukumu ya kuwapelekea huduma watu wa magoma na Mimi sijui kama itarudi ama hairudi naweza nisiweke asilimia mia moja kuwahudumia watu wa magoma kwa hiyo maendeleo yao yanarudi nyuma kwa kiasi kikubwa sana bila swala la msingi kwa hiyo mwenyekiti nitoe ushauri kama ni vikao vikaliwe kwa wakati na kama hawaji itolewe taarifa kama nyie ni watu wavijiji watabaki vijijini na kama wamjini wabaki mjini;Alisema Mhe Alfred Kimea.

Mbali na hilo pia Mhe Kimea alizungumzia changamoto ya kijiji cha kwemasimba ambacho kipo karibu na korogwe mjini ambapo kiserekali inahudumiwa na watu wa korogwe mjini kwa hiyo hawaingii kwenye vikao vyote vya manunuzi juu ya vijiji vyao

Kutoka kwemasimba kwenda korogwe vijijini ni zaidi ya masaa nane lakini kutoka kwemasimba kuja korogwe mjini ni dakika 30 hivyo naomba swala hili lifanyiwe haraka ili maendeleo ya wananchi yapatikane kwa wakati.

Waziri Ummy

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Tanga ambae pia ni waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu alikiri kuwepo na changamoto na kusema kuwa utaratibu lazima ufwatwe na kusisitiza kuwa ni nani atajadili korogwe mji anaetaka kuchukua au korogwe vijijini anaetaka kupokea.

Mhe Ummy alisema Lengo letu kama serekali ni kusogeza huduma kwa wananchi, wananchi tunawatesa magoma tatizo lipo na tumekaa tunajiita viongozi sio vizuri hatuwatendei haki tutoke kwenye fitna.

"Kwa hiyo mwenyekiti kikao chako lazima kitoke na maamuzi amesema vizuri mh Kimea na nimependa amekuwa muwazi ndio hali halisi magoma tatizo lipo na kama ni korogwe vijijini wataanza mchakato wa kuachia waende wakaanze kwenye ngazi ya vijiji kata watuletee mrejesho kama ni mji wanataka kuchukua nao wafanye hivyohivyo mwisho wa siku sisi ndio viongozi jamani tuwapunguzie mzigo wananchi wa magoma tunawatesa ;Alibainisha Mh Ummy.

                 Rc Malima 
Mkuu wa Mkoa Wa Tanga Adam Malima aliongeza kuwa jambo hilo ni muhimu sana kupata ufumbuzi ili kuwapatia wananchi huduma na kusema kuwa atakachofanya ni kupata mgao wa geographia ukoje ili alitewe huo mpango na wote waupitie na mchakato wa kurudisha jambo hilo kwenye mamlaka husika za maamuzi  uendelee.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI