Header Ads Widget

JAMII TUMIENI VIFAA VILIVYO NDANI YA MUDA KULINDA AFYA ZENU

 

Mkuu wa utafiti,TAEC,DKt.Shovi Sawe

Jamii imetakiwa kuacha tabia ya matumizi ya vitu vilivyopitwa na muda hasa mashine za mionzi(Scanner) ili kulinda usalama wao wa  afya pamoja na mazingira inayoweza kuathiriwa na mionzi.Mwandishi Teddy Kilanga MDTV Arusha 

Akizungumza mmoja wawashiriki  wa Mafunzo ya matumizi sahihi ya mionzi kutoka Zanzibar,Mohamed Bilali alisema  hapo awali walikuwa wanatumia mashine za ukaguzi(scanner) bila kufahamu madhara na usalama wa afya zao mahali ulipo

Bilali alisema kwa sasa wamepewa mafunzo hayo wamekuwa na usalama mkubwa na watakaporudi katika mahali pa kazi watafanya kazi kwa weledi pamoja na kujikinga zaidi kwani kupitia elimu hiyo waliyoipata wametambua namna ya kujilinda na kuwalinda wengine wasizulike na mionzi ya mashine hizo.

"Pia jamii inatakiwa ijifunze masuala haya ya mionzi pamoja na sheria  kwasababu kunatabia ya kuchukua vitu ambavyo vilishakwisha muda wake na kuvitumia kwani usalama wake ni mdogo hivyo naishauri  ni vyema tukatumia vitu ambavyo vipo ndani ya muda ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza,"alisema Bilali.


Kwa upande wake Mkuu wa utafiti na Mafunzo wa  Tume ya nguvu za Atomic Tanzania(TAEC)Dr.Shovi  Sawe alisema mafunzo hayo  yametolewa  kwa watumiaji wa vyanzo vyanzo vya mionzi ambayo yanatekelezwa  kwa mjibu wa sheria  ambao washiriki ni takribani 19 kutoka kundi la wafanyakazi wa migodi,

"Lengo ni kuwajengea uwezo namna ya kujikinga katika utendaji kazi wao katika vyanzo vya mionzi kwa matumizi salama pamoja na kuwakinga wengine kwa njia nzuri ya kulinda mazingira pamoja na kuwaelekeza njia nzuri ambavyo vyanzo hivyo vikishakwisha muda wake kutumia njia sahihi kwa lengo la kuwa salama,"alisema Mkuu huyo.

Aidha Dkt.Sawe alisema baada ya vyanzo hivyo kuisha muda wake utaratibu watatakiwa wavirudishe katika TAEC kwa ajili ya uhifadhi katika stoo ya kitaifa au kurudisha kwenye nchi waliyoitoaka ili wakahifadhi.


Dkt.Sawe alisema mionzi ni moja ya manufa makubwa katika jamii kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi lakini isipotumika vizuri inaweza leta athari  ndio sababu ya kukumbushana namna ya kuchukua hatua sahihi ili kuhakikisha usalama kwa wafanyakazi ,raia pamoja na mazingira.

Kaimu Mkurugenzi wa TAEC,Dkt.Regimius Kawala alisema katika masuala ya usalama ni vyema mtaalamu wa mionzi akafahamu mazingira aliyopo ya utendaji kazi wake pamoja na kuhifahamu mashine anayoitumia ili kuepuka athari zinaweza kujitokeza zinazosababishwa na kutofahamu kifaa anachotumia.

"Watumishi wa kwenye migodi unapaswa kufahamu mazingira kama vile aina ya miamba yenye mionzi ya juu lengo ni kuhakikisha usalama wa mtaalamu mwenye pamoja na kuwalinda wengine wasipate madhara yatokanayo na mionzi kwani hali hubadilika,"alisema Dkt.Remigius.

Dkt.Remigius alisema kuna baadhi ya makosa ya kibinadamu ambayo husababisha na hali ya mazingira kubadilika hivyo ni vyema wataalamu hao wa mionzi wakachangamkia fursa na huduma zinazotolewa na TAEC kwa ajili ya kujali afya zao na za wengine.

Aliongeza kuwa wataalamu hao ni vyema wakazingatia suala la utii wa sheria pamoja na kujali mazingira ya mtaalamu wa mionzi na ya wengine na hakikishe zoezi analolifanya lisiwaumize wengine kwani teknolojia hiyo italeta madhara kwa kutofuata sheria.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI