Header Ads Widget

BREAKING :AJALI YAUA 14 WAKIWEMO WAANDISHI WA HABARI 5



WATU 14 wakiwemo waandishi wa habari 6  wamepoteza maisha katika ajali iliyohusisha magari mawili ikiwa moja  la abiria na jingine lililokuwa limebeba waandishi wa habari mkoa wa Mwanza wakitokea Mwanza kuelekea Ukerewe kupitia Bunda, Mara leo Jumanne 11, 2022.

Taarifa za awali zilizotolewa na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza, Edwin Soko imeeleza kuwa tukio hilo limetokea katika Wilaya ya Busega, Simiyu baada ya gari hilo lenye namba za usajili STK 8140 mali ya Serikali kugongana na gari la abiria aina ya Toyota Hiace.

Taarifa za awali

Gari la waandishi wetu wa Mkoa wa Mwanza lililokuwa kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza limepata ajali eneo la Busega lilikuwa linaelekea Ukerewe kwa kupitia Bunda.


Nineongea na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ng. Gabriel amethibitisha kutokea taarifa za watu watano waliokuwa kwenye gari hilo lililobeba waandishi kufariki.


Majina ya wenzetu hao tutayatoa kadri tutakavyofuatilia. Kwa sasa Mkuu wa Mkoa nae anaelekea eneo la tukio nasi pia tunajipanga kwenda eneo la tukio.


Naomba tuwe watulivu kwa wakati huu, wakati team yetu na ya Mkuu wa Mkoa tunafuatilia tukio hilo.


Edwin Soko

Mwenyekiti

Mwanza Press Club

11.01.2022.


TAARIFA YA AJALI ILIYOHUSI GARI LA SERIKALI NA HIACE NA KUSABABISHA VIFO


1. WP 11158 DC JOHARI SAAN

2. HUSNA MLANZI- ITV

3. VAN CHARLES- ICON TV

4. ABEL NGAPEMBA- AFISA HABARI MKOA

5. ANTHONY CHUWA -HABARI LEO DIGITAL

6. STEVEN MSENGI- AFISA HABARI UKEREWE

7. PAUL SILANGA- DEREVA

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS