Baraza kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA)Mkoa wa Kilimanjaro limetoa tamkoa Kwa waumini wote kufanya maombi ya kuomba mwenyezi mungu kuiondolea nchi ukame na majanga mbalimbali.....Na Rehema Abraham Kilimanjaro
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Bakwata mkoa shekhe wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mlewa Shabani Kimwaga amesema kuwa ametoa tamko kutokana na tamko lililotolewa na Mufti Mkuu wa Tanzania Shekhe Abubakar Zuberi lililowataka viongozi wa mikoa yote kufanya maombi ya kuomba mvua kutokana na hali ya nchi kuwa mbaya.
Aidha amesema kuwa matumaini yamekuwa madogo kwa watu wanaotegemea kupata kipato chao kwa njia za kilimo pamoja na wanyama, ambao wanakosa majani .
"Kwa hiyo Mh. Mufti wa Tanzania alitoa tamko hili kuwataka viongozi wake wote kuanzia ngazi ya Taifa mpaka ngazi ya msikiti kufanya maombi maalum kwa ajili ya mvua Sasa kwa kufuata amri hii ,ni wajibu wetu sisi Kama viongozi wa mkoa wa Kilimanjaro kuanza utekelezaji mara moja kwa sababu mkubwa wetu amekwisha kutuagiza kufanya hivyo ,hivyo nani ninatoa tamko hilo kunukuu tamko la mh.Mufti wa Tanzania kuagiza kwamba Kila msikiti katika mkoa wa Kilimanjaro wafanye Dua ya kunuti na Nia yake ni kumuomba mwenyenzi Mungu atuondoshee ukame huu kwa kutunyeshea mvua "Alisema Kimwaga.
Katika hatua hatua nyingine amewataka wananchi kuchanja kwani Kuna umuhimu wa watu kuchanja kutokana na awamu ya nne ya ugonjwa wa COVID 19 ambayo inaonekana kuwa mbaya zaidi kuliko za awamu zote zilizopita .
"Kwa hiyo mimi natoa wito Kama Kiongozi wenu Mkuu kwenye mkoa huu wa Kilimanjaro ,kwa wale ambao ni wabishi kuchanja wachanje kwani Kuna watu ambao tayari walishachanja na mpaka Leo ni wazima na hawajapata shida yeyote"Alisema Kimwaga.
Amesema kuwa chanjo hizo hazina madhara kwani watu walishachanjwa huko nyuma chanjo ya magonjwa mbalimbali Kama polio,Ndui ,maradhi ya pepopunda ,ugonjwa wa homa ya inni ,na manjano lakini hawakuadhirika kwa chochote.
Kwa upande wake Shekhe wa wilaya Rombo Bakari Mbago amesema kuwa wameyapokea maagizo yaliyotelewa hivyo wanaenda kuyafanyia kazi .
0 Comments