Jeshi la zimamoto mkoani Kagera limethibitisha kuokoa maisha ya mtoto mchanga wa kiume anayesadikika kuwa na umri wa siku mbili hadi tatu aliyetupwa chooni katika shule ya msingi Rukajange iliyoko wilayani Karagwe mkoani Kagera......Na, Titus Mwombeki-MDTV BUKOBA.
Akiongea na Matukio Daima Media leo ofisini kwake kaimu kawanda wa jeshi la zimamoto mkoani Kagera Thomas Majuto amesema kuwa walipokea taarifa za tukio decemba mosi mwaka huu majira ya saa nnne na robo asubuhi baada ya kupokea taarifa ya tukio hilo kutoka kwa Mwananchi(hakutajwa majina) aliyekuwa anapita katika maeneo ya shule hiyo na alisikia sauti ya mtoto mchanga akilia kutokea chooni na baada ya kupokea taarifa hizo ndipo jeshi la polisi wilaya ya Karagwe liliwahi katika eneo la tukio na kweza kuokoa maisha ya mtoto huyo.
“ Baada ya kupokea waarifa za tukio hilo askari wa kituo cha zimamoto wiyaya ya Karagwe waliweza kukimbia mpaka katika eneo la tukio na kuanza kubomoa choo alipotupwa mtoto huyo na mwishowe walifanikiwa kumtoa akiwa hai na kumkimbiza katika hospitali ya rufaa ya Nyakahanga iliyoko wilaya ya Karagwe kwaajiri ya huduma ya kwanza na mpaka sasa mtoto huyo ameifadhiwa hospitalini hapo huku uchunguzi wa kumtafuta mama mzazi wa mtoto huyo ukiendelea ili aweze kufikishwa katika vyombo vya sharia”
Ameongeza kuwa kutokana na tukio hilo mpaka leo asubuhi wamepokea taarifa kuwa kuna mama mmoja ambaye ananyonyesha mtoto mchanga amejitokeza akiomba kumtunza mtoto huyo.
“Tumeweza kufahamishwa pia, kuwa kuna mama mmoja anayenyonyesha amejitokeza akiomba kumtunza yule mtoto ili awe ananyonyesha watoto wawili na sisi kama jeshi la zimamoto mkoani Kagera wazo hilotumeliacha kwa idara ya Ustawi wa jamii wilaya ya Karagwe walishughulikie ili waweze kutoa idhini na huyu mama aweze kumchukua mtoto huyo ili aweze kumpa huduma ya kumnyonyesha"
Aidha kamanda Majuto amewaomba wananchi mkoani Kagera kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pale wanapoona mtu ambaye walikuwa wakimuona akiwa na ujauzo au mtoto lakini mwishowe mtu huyo kuonekana hana mtoto wala ujauzito ili kusaidia kutokomeza matukio haya.
0 Comments