Header Ads Widget

WATAALAM WA UCHUNGUZI WA MAGONJWA YA MIONZI ZAIDI 100 WANOLEWA



Mkurugenzi wa teknolojia za huduma za kiufundi Dkt.Remigius Kawala amesema kati ya kaguzi 655 za matumizi ya mionzi kwa wataalam ibainika uelewa mkubwa wa mafunzo yanayotolewa na serikali kila mwaka kupitia Tume ya Mionzi Tanzania(TAEC) umeongezeka......Na Teddy Kilanga_Arusha




Akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa kwa wataalam wa uchunguzi wa magonjwa ya mionzi nchini wapatao 110 yaliyofanyikia jiji la Arusha ,Dkt.Kawala alisema wataalamu hao wameanza kuelewa umuhimu wa mafunzo hayo kwa kufanya na kutenda kulingana na usalama unavyotaka.



"Kwa hiyo mafunzo haya hayapo kwa sababu ya mazoea bali ni kwa ajili ya kuendeleza ule utamaduni mzuri wa kuwa na udhibiti salama wa hizi mashine za mionzi pamoja na kuindesha kwa umakini zaidi,"alisema Dkt.Kawala.



Alisema wanafanya mafunzo hayo ili kuhakikisha wataalamu wa tiba na uchunguzi wa magonjwa kwa kutumia mionzi wanapata elimu ya usalama wa vyanzo vya mionzi




Aidha alisema pia wanaendeleza namna njema yakuwa na viasili au vifaa vya mionzi kwa ajili kuwalinda pamoja na kulinda wateja wao ambao ni wagonjwa.



Naye Mkuu wa kitengo cha utafita na mafunzo kutoka TAEC ,Dkt.Shovi  Sawe alisema wamekuwa wakitoa mafunzo kwa makundi mbalimbali ambayo yanatumia vyanzo vya mionzi ikiwa ndani ya wiki hii kuanzia Desemba 13 hadi 17,2021 watakuwa na kundi la afya.



"Ndani ya wiki hii tutakuwa na kundi la afya linalotumia mionzi katika uchunguzi na tiba za magonjwa kwa kutumia vyanzo vya mionzi kwani mafunzo ni muhimu katika nyanja zote kwa lengo la huduma hiyo kutumika vizuri,"alisema Dkt.Sawe.




Aliongeza kuwa mionzi isipotumika vizuri ni hatari kwa afya ya binadamu kunzia watumiaji na ambao hawatumii hivyo wamelenga kujenga uwezo katika kinga ya mionzi na ili waweze kupata faida wanayoitegemea kwenye huduma hiyo inabidi wagonjwa walindwe pamoja na wataalamu wenyewe kujilinda dhidi ya madhara mabaya yanayoweza kutokea kutokana na mionzi.



"Ikumbukwe kuwa mionzi imedhibitika kuwa na  faida ambazo chunguzi za aina nyingine  haziwezi kufanya mfano kupiga picha ya mguu uliovunjika kwani mionzi imethibitika kuwa na ufanisi mkubwa kuliko aina nyingiza za uchunguzi,"alisema Dkt.Sawe.





Kwa upande wa baadhi ya washiriki hao wa mafunzo,Hellen Lisakafu na Daniel Mariki walisema mafunzo hayo yamekuwa chachu ya kujilinda pamoja na wanaowahudumia katika kutumia mionzi hivyo tunaishukuru Tume ya Mizonzi Tanzania kwa kuhakikisha wanakuwa salama.



"Mafunzo haya yanatija kubwa kwetu hasa kwetu sisi watumiaji wa teknolojia ya mionzi kwani kwa kipindi kifupi katika mwaka huwa kunautaratibu ambao TAEC wamejiwekea katika kupitia kufanya ukaguzi za mashine ambazo zinatumika hivyo wakiwa wanapita huwa tunapata maelekezo mbalimbali ya matumizi ya vifaa,"alisema Mariki.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI