Header Ads Widget

SERIKALI YABORESHA MIUNDOMBINU YA CHUO CHA MAENDELEO YA JAMII TENGERU

 



Naibu waziri wa afya ,maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto,Mwanaidi  Khamis amesema serikali imeweka kipaumbele katika kuboresha mazingira ya kujifunza na kujifundishia katika taasisi na vyuo ili kutoa mafunzo yanayokidhi mahitaji ya soko.......Na Teddy Kilanga _Arusha



Akizungumza katika Taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru(TICD) alipotembelea mradi wa ujenzi wa bweni la wasichana pamoja na kumbi pacha,Naibu waziri khamis alisema amefurahishwa na maendeleo ya ujenzi huo ambao umegharimu takribani sh.bilioni 2.6 kwani serikali imeshatoa fadha zote za ukamilishwaji wa majengo hayo.




Hata hivyo alitoa rahi kwa bodi ya taasisi hiyo kusimamia fedha  hizo vizuri na kukamilisha mradi kwa wakati  ili wanafunzi hasa jinsia ya kike wapate mahali salama na bora wakati wote wa masomo yao.



"Serikali yetu inasisitiza utoaji wa elimu kwa inayojenga ujuzi hivyo naipongeza taasisi hii kwa kuagiza dhana ya uanagenzi,ubunifu na ushirikishwaji wa jamii katika mitaala ya mafunzo kwani hii ni hatua kubwa katika jitihada za kuhakikisha Maafisa maendeleo ya jamii wanapata stadi za kazi,"alisema.



Aliongeza kuwa ni vyema wadau wa mahali pa kazi kama vile mamlaka za serikali ,asasi za kiraia ,mashirika na makampuni mbalimbali kutenga nafasi za uanagenzi ili wanafunzi wa taasisi ya maendeleo ya jamii kuweza kutatua changamoto za ajira.



Alisema ni wazi kuwa serikali pekee au sekta binafsi hazina uwezo wa kuajili wahitimu wote wa elimu ya juu kwani dhana hiyo ya uanagenzi ni njia mojawapo ya suluhisho la ukosefu wa ajira kwa kuwa wahitimu wanapata ujuzi wanaweza kutumia kujiajiri na hata kuajiri wengine.



"Napenda kuwahakikishia kuwa mimi mwenyewe binafsi na wizara yangu kwa ujumla tutaendelea kushirikiana na bodi katika utatuzi wa changamoto zote zinazokabili taasisi yetu,"alisema Naibu waziri huyo.




Naibu waziri huyo alisema kama sehemu ya taasisi hiyo kuwa kongwe wizara itajitahidi kuhakikisha kuwa fedha za miradi ya maendeleo zinapatikana kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala,hosteli za wanafunzi na kumbi za mihadhara kadri ya bajeti ya uchumi wa nchi hii inavyokuwa.



Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi uendeshaji wa taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru,Dkt.Rosemarie Mwaipopo alisema taasisi imekuwa ikiendelea kutekeleza majukumu yake kulingana na mpango mkakati wa mwaka 2017/2018 hadi 2022/2023.



"Tunashukuru serikali yetu pendwa kwa kutupatia fedha za maendeleo kwa ajili ya kumbi pacha na hostel za wasichana hivyo tumeendelea kutekeleza miradi hiyo ikiwa sasa hivi tunajipanga kuweka vitendea kazi na huduma mbalimbali katika majengo hayo ili kuendeleza malengo yaliyotarajiwa,"alisema Dkt.Mwaipopo.



Aidha alisema taasisi hiyo inatarajia kuanza ujenzi wa jengo la utawala,kituo cha kimataifa cha ubunifu na kumbi ndogo za mihadhara lengo ni kuboresha zaidi utoaji elimu na maarifa ya maendeleo ya jamii kwa vitendo na pia kwa njia shirikishi.



Naye Mkuu wa Taasisi hiyo,Bakari George alisema kutokana na mabadiliko mbalimbali nchini kuhusu masuala ya teknolojia wamejipanga kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa wataalamu wa maendeleo ya jamii walioko sehemu za kazi kutoka sehemu mbalimbali lengo ni kuwasaidia namna ya kutekeleza majukumu yao kwa wakati huo.



"Kuanzia mwakani tutaanza kutoa mafunzo haya ili yawasaidie kwenye utekelezaji wa shughuli zao kwa kuzingatia dhana ya ubunifu katika maendelei ya sayansi na teknolojia,"alisema Mkuu huyo wa Taasisi.



Dkt.Bakari alisema wanamshukuru Rais Samia Suluh Hassan kwa kuwapatia fedha za ujenzi huo wa hostel ya wasichana na kumbi pacha ikiwa mradi wa bweni umefikia asilimi 55  ambapi unatarajiwa kukamilika Aprili 30,2022.



Mkuu huyo alisema Mradi wa kumbi pacha wenyewe upo kwenye asilimia 70 na unatarajiwa kukamilika februari 14,2022 kwani hapo awali walikabiliwa na changamoto wa hupatikanaji wa vifaa pamoja na kukatika kwa umeme.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI