SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imewataka Wananachi Visiwani humo kushirikiana na Serikali katika kutekeleza Uchumi wa Buluu.
Wito huo umetolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi wakati akifungua mkutano wa kwa njia ya Mtandao wa Zoom ambao ulikuwa unazungumzia mada ya Falsafa ya Uchumi wa Bluu kwa Maendeleo ya Tanzania.
Mkutano huo umeandaliwa na Watch Tanzania Agency na kuwashirikisha Wadau mbalimbali wa Manedeleo Nchini.
Rais Dkt Mwinyi alibainisha kuwa ili Zanzibar iweze kuendelea na kunufaika na Sera ya Uchumi wa Buluu Wananchi hawana budi kuunga na Serikali katika kutekeleza Sera hiyo.
“Wito wangu kwa Wananachi wa Zanzibar (Unguja na Pemba) ni lazima sote tuwe sehemu ya Uchumi wa Buluu kutoka kuwa una faida kubwa kwa Wananchi pamoja na Serikali,” alisema.
Hata hivyo Dkt Mwinyi alitoa wito kwa watendaji wa Serikali kuwa na muoamko na kupokea Sera ya Uchumi wa Buluu kwa faida ya Nchi
“Wafanyakazi wa Serikali lazima sote tupokee na twende nayo pamoja Sera ya Uchumi wa Buluu,” alisema Dkt Mwinyi.
Katika Mkutano huo umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanziabr, wakiwemo Mawaziri, Viongozi wa Taaisisi za Serikali na Sekta Binafsi pamoja na Wananchi kwa Ujumla.
0 Comments