RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ni kuhakikisha Visiwa Vya Unguja na Pemba vinakuwa kwa kasi Kiuchumi na kuwanufaisha Wananchi wake.
Kauli hiyo ameito leo Wakati Akifungua mkutano kwa njia ya Mtandao wa Zoom ambao ulikuwa unazungumzia mada ya Falsafa ya Uchumi wa Buluu kwa Maendeleo ya Tanzania.
Katika Mkutano huo umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanziabr, wakiwemo Mawaziri, Viongozi wa Taaisisi za Serikali na Sekta Binafsi pamoja na Wananchi kwa Ujumla.
Rais Dkt Mwinyi amesema kuwa azma ya Serikali ni kuhakikisha Uchumi unakuwa na kuwanufaisha Wananchi wake wote wa Unguja na Pemba.
Katika Maelezo yake Dkt Mwinyi amefafanua kuwa Sera ya Serikali ni kufanya Kisiwa cha Pemba nacho kinakuwa kwa kiuchumi na kuenda sambamba na kisiwa cha Unguja.
“Azma ya Serikali ya Serikali ni kufanya Kisiwa cha Unguja na Pemba vinaenda sambamba katika ukuaji wa Uchumi na ili tuweze kufanikiwa katika sera zetu, tunahitaji ushirikiano wa Wananchi na Serikali,” alisema.
Hata hivyo Dkt Mwinyi alisema kuwa, Serikali YA Mapinduzi ya Zanzibar imeazimia kuwawezesha Wavuvi kwa kuwapa Elimu ya Jinsi ya kufanya kazi ya Uvuvi kisasa zaidi.
“Mbali na hayo tumeazimia kuwawezesha Wavuvi kwa kuwapa mitaji na kuwapa masoko ya uhakika ambayo yatapatikana kwa kuwavutia Wawekezaji,”
Hata hivyo Dkt Mwinyi alisema kuwa, Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wanaendelea katika mazungumzo mbalimbali ya kutatua changamoto za Muungano.
“Serikali zetu mbili ya Bara na Visiwani tumeendeleza Mazungumzo yaliyokuwa yanafanywa juu ya kutatua changamoto za Muungano na karibu changamoto nyingi zimepata ufumbuzi zilizobaki ni chache.
0 Comments