Amesema hayo mganga wa hospitali ya maalum ya magonjwa ambukizi kibongoto Drt. Leornard Subi iliyopo Siha mkoani Kilimanjaro wakati alipokuwa akiongea katika katika zoezi la uzinduzi wa Afya marathon inayotarajiwa kufanyika tarehe 26 mwezi wa 12 iliyoambatana na zoezi la upandaji miti katika hospitali hiyo.
aidha amesema kuwa ugonjwa huo umekuwepo kwa chini chini lakini inaongoza kwa kuuwa watu mbalimbali Kila Siku na hiyo inatokana na watanzania kutopewa elimu juu ya ugonywa huo.
Sambamba na amewapongeza wadau waliokuja na mpango wa Siha marathon agenc itakayosaidia kutoa elimu kwa wananchi na kusema taasisi za Serikali na zisizo za Serikali zishirikiane katika kuelimisha wananchi juu ya mapambano ya ugonjwa wa kifua kikuu.
"kwa bahati mbaya ugonjwa wa Kifua kikuu unawathiri watu wanaoishi kwenye familia duni ,watu waliopo kwenye migodi ,maeneo ya magereza,misongamano na kwa bahati mbaya Sasa Kuna baadhi ya wagonjwa wanaoupata usugu wa madawa na ndio maana tunajenga maabara ya kisasa ,na kuendeleza sayansi ya kitafiti na uchunguzi "Alisema.
Amesema kuwa mbio hizo za marathon zomeambatana na ujumbe wa afya ya namna gani ya kuweza kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu
Amesema kuwa ugonjwa wa kifua kikuu ni ugonjwa wa muda mrefu na sio kitu kipya kwani hospitali hiyo ya kibongoto ilianzishwa mwaka 1926 ambapo mwaka 1952 ikapewa fursa ya kuwa hospitali ndani ya wilaya hiyo.
Akizungumza wakati wa ugawaji wa miche hiyo Mwenyekiti wa taasisi ya Siha Sports Agency Sellina Mkonyi amesema kuwa ili kuendana na dhima ya mbio izo za Siha Afya marathon jamii inapaswa kuwa mstari wa mbele kwenye utunzaji wa mazingira ukizingatiwa kipindi hikili chenye ukame kwenye maeneo mengi kwa ukataji wa miti ovyo na uharibifiu wa vyanzo vya maji kwani miti 3,000 itapelekwa hospitali ya Kibong'oto na 5,000 itaoteshwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Siha.
Katika kuelekea madhimisho ya Siha Afya Marathon Wakala wa Misitu (TFS) wametoa miche 8,000,ambapo miche 3,000 itapandwa kwenye hospitali ya Kibong'oto na maeneo mengine ili kutunza mazingira katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kilimanjaro.
0 Comments