Header Ads Widget

RC ARUSHA AOMBA MSHIKAMANO WA MADHEHEBU YA DINI NA SERIKALI KATIKA KUTOKOMEZA UKIMWI

Mkuu wa moa wa Arusha John Mongela akihutubia katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani yaliyofanyika mkoani Arusha


Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela ameyaomba madhehebu ya dini kushikamana na serikali katika kuhakikisha wanatokomeza ugonjwa wa UKIMWI kwani ugonjwa huo bado ni changamoto katika jamii.MWANDISHI NAMNYAK KIVUYO, MDTV ARUSHA


Mongela alitoa ombi hilo katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani yaliyoadhimishwa kiwilaya katika eneo la Kilombero mkoani Arusha ambapo alisema kuwa ni vema madhehebu ya dini yakaunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali katika kupambana na UKIMWI.


“Sichochei matumizi ya Kondom lakini tunataka kupingana na ugonjwa huu na pengine kwa hulka za kibidamu hutufuati yale tunayofundishwa katika nyumba za ibada lakini mimi naamini mshikamano wa madhehebu, mshikamano waserikali utafanya  haya maambukizi ya UKIMWI tuyakabili,” Alisema Mongela.


Alifafanua kuwa madhebu ya dini yana programu mbalimbali za kusaidia hivyo Wana haja ya kuendelea kushikamana  ili mafanikio yaweze kuwa makubwa lakini pia serikali inatambua juhudi kubwa zinazofanywa na madhehebu ya dini katika kukabiliana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.


Sambamba na hayo pia aliitaka jamii kuunga mkono suala la kupima, kujua  afya zao, na kufuata masharti ya kujikinga na maambukizi lakini pia Kuacha tabia za kizamani za unyanyapaa kwani kwa sasa hivi mtu mwenye maambukizi anamchango sawa au zaidi ya yule ambaye hana maambukizi.


Kwa upande wake Tajieli Mahenga kaimu afisa maendeleo ya jamii jiji la Arusha alisema kuwa kwa mwaka 2021 wameweza kuelimisha kata zote 25 za jiji la Arusha juu ya maambukizi na namna ya kujikinga na maambukizi hayo ,  kugawa Kondom za kike na kiume  laki 9 na 80 huku watu laki 3 na 70 mia 603 wameweza kujitokeza kupima afya zao  na wenye maambukizi wapatao 2150 wameingizwa kwenye tiba na matunzo katika vituo vya afya vya jiji la Arusha.


Alifafanua kuwa wameweza kuongeza vituo vya klinik kutoka 17 hadi 22 pamoja na kiwango cha kufubaza UKIMWI kimeongezeka kutoka asilimia 85 hadi 95 ambapo pamoja na mafanikio hayo pia wanakabiliwa na changamoto ya kiwango cha maambukizi ya UKIMWI kuongezeka kutoka asilimia 2.3  mwaka 2019/2020 hadi kufikia asilimia 2.8 2020/2021.


“Kiwango hiki kinaongezeka kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo upimaji wa makundi maalum ambayo ni vijana walioathirika na madawa ya kulevya, madada poa na makundi mengine huku  nyingine ikiwa ni kuzingatia vigezo vya  upimaji ambao umeongeza ufanisi wa upimaji na watu wengi wamehamasika  kujijitokeza kupima,”Alisema Tajieli.

Tajieli Mahenga kaimu afisa maendeleo ya jamii jiji la Arusha


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI