Mkuu wa Wilaya ya Moshi Saidi Mtanda ameitaka jamii kuendelea kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Ukimwi na magonjwa mengine ya mlipuko Kama COVID 19 kwani Bado yapo na yanaendelea kuuwa watu.Mwandishi Rehema Abraham
Mtanda ameyasema hayo Leo katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyoandaliwa na mashirika mbalimbali yanayojishughulisha na masuala ya Afya kwa jamii ikiwemo ugonjwa wa Ukimwi yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mkuu wa mkoa mkoani Kilimanjaro.
Mtanda amesema licha ya kuwepo kwa mlipuko wa magonjwa mengine kama Uviko 19 bado jamii inapaswa kutambua na kuzingatia kujikinga na maambukizi ya Ukimwi huku akiwataka wenye maambukizi hayo kutokata tamaa.
Grace Momanyi ni Mratibu wa UKIMWI Manispaa ya Moshi Moani Kilimanjaro amesema katika jitihada za kupambana na maambukizi ya virusi vya ukimwi wamekua wakitoa elimu mbalimbali kwenye jamii ili kupima na kujitambua hali zao ili iwasaidie kufanya shughuli za maendeleo kwa ufanisi zaidi.
Amesema Manispaa ya Moshi ina vituo 35 vinavyotoa huduma za upimaji na vituo 19 vvya huduma ya tiba na matunzo na kwamba kwa mwaka huu wamefanikiwa kupima watu zaidi ya elfu 60 kati ya hao wanaume wakiwa elfu 25,202 huku wanawake wakiwa elfu 35,465 ambapo wanawake zaidi ya 800 na wanaume zaidi ya 500 waligundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Hata hivyo kutokana na maambukizi hayo jamii imetakiwa kujikinga na maambukizi hayo ili kulinda nguvu kazi ya taifa kwani kundi kubwa linalotajwa kupata maambukizo ni kuanzia miaka 15-45 .
0 Comments