Mkurugenzi Wa Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro akipokea kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo Halima Okash Mizinga 85 kutoka kwa WAKALA wa Huduma za Misitu (TFS) ambayo itagawiwa kwa vikundi sita vya ufugaji nyuki vinavyofanya shughuli zao za ufugaji nyuki vya kuzunguka hifadhi.
Akizungumza wakati wa kukabidhi Mizinga hiyo katika ofisi ya Kituo Cha Msitu wa mazingira asilia Mkingu, Kamanda Msaidizi Rasilimali za Misitu kutoka TFS Bernadetha Kadala amesema lengo na dhumuni la ugawaji wa mizinga hiyo ni kutia chachu na kuchochea ufugaji endelevu wa nyuki katika Msitu wa mazingira Asilia Mkingu.
Aidha Kadala amesema thamani ya mizinga hiyo 85 ni Sh.10,200,000 amekabidhi mizinga ya nyuki katika Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro kwa lengo la kuhamasisha ufugaji nyuki endelevu na kuleta chachu na kuchochea kilimo cha ufuguji nyuki katika Hifadhi Ya msitu Asilia Mkingu.
Hifadhi ya msitu wa mazingira Asilia Mkingu iliyo chini ya Wakala Wa Huduma za Misitu Tanzania ni miongoni nwa hifadhi 20 za misitu ya serikali kuu zilizopandishwa hadhi ya uhifadhi kuwa Hifadhi za mazingira nchini.Hifadhi hiyo inazungukwa na vijiji 25, vyenye idadi ya wakazi wapatao 61,000 wanaojishughulisha na uzalishaji mali ikiwemo kilimo na ufugaji.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mvomero Hassan Njama Hassan ametoa shukrani kwa TFS kwa kuona umuhimu wa kutoa mizinga hiyo ambayo inakwenda kubadilisha ufugaji nyuki kutoka ule wa mazoea na kuwa wa kisasa, na kwamba mizinga hiyo italindwa na kutunzwa ili kuleta tija.
0 Comments