Wakala wa huduma za misitu (TFS) wametoa msaada wa mizinga ya nyuki 85 yenye thamaani zaidi ya milioni kumi kwa vikundi sita vinavyozunguka hifadhi ya mazingira asili Mkingu wilaya ya Mvomero mkoa Morogoro
Akizungumza mara baada ya kukabidhi mizinga hiyo meneja msaidizi Rasilimali za misitu kanda ya Mashariki Benadetha kadala amesema mizinga hiyo inafaida kubwa katika jamii hasa utunzaji wa mazingira
Benadetha anasema kwa sasa changamoto kubwa kwa wakulima ni ukosefu wa mvua kunyesha hali ambayo imetokana na mabadiliko tabia nchi ambayo yamesababishwa na watu kufanya uharibifu wa misitu kama kulima,kukata miti na kuchoma mkaa katika hifadhi za msitu.
Anasema msitu wa asili wa Vikingu unajumla ya mito 25 imekua na faida kwa watu wa Mvomero na maeneo jirani hivyo mzinga hiyo itasaidia katika utunzaji wa mazingira
"wakulima wa mvomero wanatumia mito hiyo katika shughuli zao za kilimo hivyo endapo msitu huu utaharibiwa kunauwezekano kutoeka changomiyo ya upatikanaji waazao hivyo jamii inatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inatunza misitu yote iliyopo"amesema Benadetha
Akitoa shukrani kwaniba ya vikundi sita vilivyopata mizinga hiyo kiongozi wa kikundi cha Mwanzo Mgumu Mwajuma Msuya anasema ufugaji wa nyuki umekua na faida kubwa kwao katika kujiingizia kipato.
Anasema licha ya kusaidia katika utunzaji mazingira lakin umeleta ajira kwa vijana wengi ambapo ameahidi kwenda kutoa elimu kwa jamii inayomzunguka kuona umuhimu wa ufugaji nyuki.
0 Comments