Header Ads Widget

PIGA KONGAMANO LA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA TGNP







































 
















TGNP 
USULI NA MUKTADHA 
MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA TAREHE 08/12/21, KATIKA KUMBI ZA MWALIMU NYERERE CONVERSION CENTER-DAR ES SALAAM
BI. LILIAN LIUNDI MKURUGENZI MTENDAJI WA TGNP 
Ndugu Mgeni rasmi Mheshimiwa Mh. Profesa Kitila Mkumbo (MB), Waziri wa Viwanda na Biashara, 
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi , wajumbe wa Bodi na Wanachama wa  TGNP, 
Ndugu Wawakilishi kutoka Taasisi za Umma na Serikali, na Wadau wa Maendeleo,
Wadau wetu wa maendeleo
Asasi za Kiraia
Vituo vya Taarifa na Maarifa na Washiriki wa GDSS 
Waalimu walezi wa Vitovu vya Jinsia mashuleni
Vyombo vya habari 
Wageni waalikwa
Tunafuraha kubwa sana kukutana nanyi katika kongamano hili maalumu kama sehemu ya maadhimisho ya kampeni ya kimataifa ya kupinga Ukatili wa kijinsia. Kampeni ambayo huadhimishwa duniani kila mwaka ifikapo tarehe 25 Novemba hadi tarehe 10 Disemba. 


Ninayo furaha na heshima kubwa sana kuwa na Mheshimiwa Profesa Kitila Mkumbo (MB), Waziri wa Viwanda na Biashara, aliyekubali kuwa Mgeni rasmi wa kongamano hili. Asante sana kwa kuacha shughuli zako zote na kutupa heshima kwa kuona umuhimu wa kuja na kuongea na wadau waliokusanyika hapa kutoka katika maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam na nje ya Dar es salaam. Tunakushukuru sana. 

Naomba pia nitambue uwepo wa wageni wote kama mlivyotambulishwa na kukaribishwa na mwakilishi wa Mwenyekiti wetu wa bodi 

Kama alivyotoka kusema mwakilishi wa Mwenyekiti wetu wa Bodi, mwaka huu maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yamejikita katika kauli mbiu ya Kitaifa isemayo- “Ewe Mwananchi: Komesha Ukatili wa Kijinsia SASA” na kauli mbiu ya kimataifa isemayo, - “Orange the World: End Violence Against Women NOW!”. 
Katika kuendeleza mijadala kuhusu kauli mbiu hizo, TGNP imejikita katika kufanya tathmini ya Utengwaji rasilimali fedha kwa ajili ya utelelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).  Kwa pamoja tutasherekea hatua za serikali na wadau zilizofikiwa katika utekelezaji wa MTAKUWWA kupitia utengwaji wa rasilimali fedha, kujadili namna ya kutatua changmoto zilizopo na kuweka mikakati ya pamoja ya kutomoza ukatili wa kijinsia nchini. 


Katika kuhakikisha usalama wa wanawake na watoto nchini, Serikali kwa kushirikiana na wadau iliandaa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) 2017/2018-2021/22, wenye kulenga kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa asilimia 50 ifikapo 2022. 
Katika kufikia azma hii, Mpango ulibainisha maeneo mahususi nane (08) ya utekelezaji. Maeneo hayo ni: Kuimarisha Uchumi wa Kaya; Mila na Desturi; Mazingira Salama katika Maeneo ya Umma; Malezi, Msaada kwa Familia na Mahusiano; Utekelezaji na Usimamizi wa Sheria; Utoaji wa Huduma kwa Waathirika wa Ukatili; Mazingira Salama Shuleni na Stadi za Maisha; na Uratibu, Ufuatiliaji na Tathmini. Afua zilizobainishwa katika maeneo haya zinaziba mianya yote inayochochea kushamiri kwa vitendo vya ukatili katika jamii. Kwa sehemu kubwa, serikali ikishirikiana na AZAKI na wadau wa maendeleo imepiga hatua katika utekelezaji wa afua za kimkakati zilizojumuishwa katika MTAKUWWA. 
Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wameweza kuchangia rasilimali fedha ili kuwezesha utekelezaji wa afua za MTAKUWWA. Katika kipindi cha mwaka 2020/21, jumla ya shilingi 2,648,422,818.00 zilitengwa na jumla ya shilingi 1,240,440,885 zimetolewa kwa ajili ya utekelezaji katika taasisi mbalimbali. Vilevile, kupitia kupitia programu ya TASAF jumla ya shilingi 107,916,895,450 zilitumika. 
Rasilimali hizo zilisaidia utekelezaji wa afua mbalimbali ikiwemo kuongezeka kwa vitou vya mkono kwa mkono vimeanzishwa katika sehemu mbalimbali nchini ili kuweza kurahisisha utoaji wa huduma kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia. Vituo hivyo vimeanzishwa Amana, 

Mwananyamala, Tumbi, Iringa, Tabora Kitete, Sekou Toure, Mbeya FFU, Simiyu, Shinyanga, Kahama, Hai, Mount Meru and Nindo. Jumla ya nyumba salama sita zimesajiliwa mkoani Arusha (faraja), Kigoma (Wote Sawa), Mara (Hope for Girls & Women in Tanzania and ACT Mara), Kilimanajaro (Network Against Female Genital Mutilation) and Manyara (Masai Girls Rescue Center).  Jumla ya madawati ya Jinsia 420 yameanzishwa katika vituo vya polisi katika maeneo mbalimbali nchini. 
Katika kuhamasisha na kutokomeza mila kandamizi, miongoni mwa hatua zilizopigwa na serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ni pamoja na kutengeneza mifumo mizuri ya kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia hasa ukatili wa watoto. Hatua ambayo imeonesha kuzaa matunda katika kuongeza uelewa kwa jamii na kuongezeka kwa matukio yanayoripotiwa kupitia namba 116. Hadi Februari 2021, jumla ya simu 1,079,891 zilipokelewa na kufanyiwa kazi. takribani wahanga 5,228 walipatiwa huduma ikiwemo kupelekwa kwenye nyumba salama, huduma za kisheria na ushauri nasaa, ukilinganisha na mwaka 2019/2020 ambapo ni wahanga 3,044 tu ndo walipata hizo huduma. 
Katika eneo la Malezi, Msaada kwa Familia na Mahusiano, hatua imepigwa na serikali kwa kushirikiana na wadau ambapo serikali kwa kushirikiana na wadau imeanzisha jumla ya mitandao ya malezi chanya 3,963 katika jamii katika mikoa mbalimbali nchini ukilinganisha na mwaka 2019/2020 ambapo mitandao 2,777 ilianzishwa. Mitandao hii hutumika kufanya majadiliano ya kirika yenye lengo la kutokomeza ukatili wa kijinsia. Pia, serikali imeenda 

mbali na kuanzisha vituo 30 kwa ajili ya kutoa huduma za elimu kwa watoto wadogo katika mikoa ya Dar es Salaam (Temeke 5 na Kigamboni 5) na Dodoma (Bahi 5, Kongwa 5, Chamwino 5, and Kondoa 5). Kutokana na huduma hiyo, jumla ya watoto children's 774,816 (375,809 Me and 399,007 ke) wamesajiliwa kupata huduma hiyo hadi Juni mwaka 2021 ukilinganisha na watoto 159,479 (82,539Me and 76,940ke) ambao walisajiliwa kabla ya mwishoni mwaka 2019/20. (Taarifa ya serikali ya utekelezaji wa MTAKUWWA-2021)

Napenda kutambua na kupongeza juhudi hizo za Serikali yetu zenye kuchangia kufikia mikataba mbalimbali ya kimataifa, kikanda na kitaifa yenye lengo la kumlinda mtoto wa kike na mwananmke dhidi ya aina zote za ukatili wa kijinsia.  

Mkataba wa Kimataifa wa Kuondoa aina zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake (1979); Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto (1989); Mpango Kazi wa Beijing (1995); Malengo ya Maendeleo Endelevu (2015); Ajenda ya Maendeleo ya Afrika Tuitakayo (2063); Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto (1989); Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Jinsia (2000); Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Mtoto (2008); Dira ya Maendeleo ya Taifa (2025); Mpango wa Taifa wa Maendeleo ya Miaka Mitano II (2016/17 - 2020/21); na Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (2015 - 2020).

Tunapozungumzia usawa wa kijinsia n suala la maendeleo na ukatili wa kijinsia ni moja ya vikwazo vikubwa kufikia usawa wa kijinsia. Jinsia ni suala la Maendeleo hatuna budi kwa pamoja kutoa kipaumbele ili kuongeza ushiriki wa wanawake wenye tija katika Maendeleo. Ni kwa mantiki hii TGNP tumeamua kuandaa kongamano 

hili kama sehemu ya kutoa fursa wadau wengine kutafakari wapi tumefanikiwa, wapi bado kuna changamoto na kupanga mikakati ya kutokomeza ukatili wa kijinsia nchini, hususani kupitia utengwaji wa rasilimali za kutosha ili kutekeleza afua mbalimbali. 

Kama kauli ya mwaka huu inayosema, hatua inapaswa kuchukuliwa SASA ya kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia na wito umetolewa kwa wananchi wote, kila mmoja katika nafasi yake.  

Kwa hayo machache niwatakie majadiliano yenye kuzaa matunda katika kuleta usawa wa kijinsia na maendeleo endelevu ya taifa letu. Niwakaribishe sana katika Kongamano hili na ni wakaribishe sana TGNP. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI