Mikoa ya kanda ziwa imetajwa kuwa miongoni mwa Mikoa inayoongoza kwa vitendo vya ukatili hapa nchini.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza mhandisi Robert Gabriel katika maadhimisho ya siku 16 ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto ambayo kwa jeshi la polisi kitaifa yamefanyikia jijini hapa.
Gabriel ameeleza kuwa kutokana na utafiti uliofanywa na ofisi ya Taifa ya takwimu (NBS) kwa mwaka 2015 na 2016 uonesha kiwango cha ukatili Mkoa wa shinyanga ikiwa ni 78%, Mara 78%, kagera 67%, Geita 63%, Simiyu 62 pamoja na Mwanza ikiwa na 60%
Hata hivyo ameitaja Mikoa ya shinyanga na Mara kuonekana kuwa na kiwango kikubwa cha ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto hali ambayo ni tofauti na ukilinganisha na maeneo mengine hapa nchini.
"Imani yangu ni kwamba maadhimisho yaliyofanyika mkoani hapa itakuwa chachu kwa wananchi na watu wenye mamlaka katika nafasi mbalimbali wakiwemo wadau wa kupinga ukatili kuhakikisha wanajipanga upya kutokomeza Ukatili huu" Alisema Gabriel.
Gabriel ameeleza kuwa hakauna Taifa litakalo kuwa imara kama kundi kubwa la watanzania hususani kwa wanawake na watoto awako katika usalama, hivyo hupelekea makundi hayo kushindwa kushiriki katika shughuli za kujenga nchi na kukuza uchumi.
"Ukatili wa kijinsia ni kikwazo cha maendeleo kwenye nyanja zote za jamii, siasa, kiuchumi pamoja na kiutamaduni," alisema Gabriel.
Amesema kuwa vitendo vya ukatili usababisha maumivu pamoja na madhara kwa wahanga wanaofanyiwa kitendo hicho na jamii kwa ujumla inayotuzunguka pia na wanaofanya vitendo hivyo ni miongoni mwa ndugu wa karibu.
ACP Faidha Suleiman kutoka jeshi la polisi kitengo cha dawati la jinsia na watoto ameeleza kuwa kitengo hicho kimekuwa kikihidumiwa na afanyakazi waliopata mafunzo ili kuhakikisha wanatoa huduma kwa usiri ili kulinda mtoa taarifa pamoja na mhanga.
Faidha ameeleza kuwa kwenye dawati la jinsia na watoto wamekuwa wakipokea watoto wa aina mbili waliofanyiwa ukatili na wanaofanya ukatili dhidi ya watoto wenzao.
Aidha ameeleza kuwa wameandaa muongozo maalum utakao wasaidia kuhakikisha wanashughulikia maswala ya ukatili kutokana na aina ya mhanga mwenyewe na mhalifu.
Afisa mwandamizi kutoka shirika la kivulini Grace Mussa ameeleza kuwa takwimu zinaonesha namna ambavyo wanachi wamekuwa na uelewa na kutonyamazia vitendo vya ukatili katika jamii.
"Kwa sababu tunaona wamekuwa wakitoa taarifa na kutofumbia macho vitendo hivyo vya uhalifu kabsa" alisema Grace.
Aidha ameitaka serikali kuhakikisha wanaweka mikakati rafiki itakayoweza kushughulikia mashauri na kufanyika vizuri ili kuweza kutokomeza ukatili na kuwepo na funzo kwa wale wote ambao wanafanya ukatili huo.
0 Comments