Header Ads Widget

MEYA WA SONGEA AELEZEA UFANISI WA MIRADI MBALIMBALI IKIWEMO YA UJENZI WA MADARASA UVIKO 19.

 



HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma imeeleza utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ya Uviko _19 inayojenga madarasa ambayo yatakamilika Desemba 10 mwaka huu.......NA AMON MTEGA, SONGEA.


Akizungumza na vyombo vya habari Meya wa Manispaa hiyo Michael Mbano amesema kuwa miradi ya ujenzi wa madarasa ambayo fedha zake zimetokana na Uviko 19 yameshakamilika kwa asilimia 95 huku miradi mingine ikiwemo ya Afya ikiendelea kutekelezwa ambayo inatarajiwa kutumia fedha zaidi ya Sh.Bilioni mbili.


 Mbano amesema kuwa katika miradi ya ujenzi wa madarasa hayo fedha zilizotolewa na Serikali ni Sh.Milioni mia sita na sitini elfu na kuwa ujenzi wake umetumika kwa kuwatumia mafundi wa kawaida ambao  husimamiwa na wahandisi wa ujenzi .


  Aidha meya huyo ameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ya Uviko 19 kwa kujenga madarasa ambayo yatapunguza tatizo la msongamano kwa wanafunzi.





  Hata hivyo Halmashauri hiyo kupitia wakuu wake wa idara imezungumzia baadhi ya idara zilivyoweza kujipanga ambapo katika idara ya mifugo na uvuvi mkuu wake wa idara Rozina Chuwa amesema kuwa wamejipanga kuanzisha kiwanda cha kuchakata vyakula vya mifugo ili kuwapunguzia  adha inayowakuta wafungaji wa mifugo mbalimbali ikiwemo kuku wa manispaa hiyo kuuziwa chakula hicho kwa garama kubwa jambo ambalo halistahili .





 Kwa upande wake mkuu wa idara wa maendeleo ya Jamii Martin Mtani amesema kuwa idara yake imejipanga kuendelea kutoa mikopo ya garama nafuu kwenye makundi matatu kwa mjibu wa kanuni ambayo ni kundi la Vinaja ,Wanawake na Walemavu ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.





  Katika Sekta ya Afya mganga mkuu wa Manispaa ya Songea Dr.Amos Mwenda amesema zoezi la uchanjaji wa chanjo ya uviko 19 unaenda vizuri huku akiwataka wananchi waendelee kuchukua tahadhari kwa kutumia kinga zinazoelezwa na watalaam wa Afya.





  Naye afisa biashara wa Manispaa ya Songea Furaha Mwangakala amesema kuwa idara yake imejipanga vema katika kuhakikisha kila mfanyabiashara anafanyia biashara zake katika maeneo husika yaliotengwa na Halmashauri hiyo.


                        

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI