Header Ads Widget

MBUNGE KIKWETE MGENI RASMI KONGAMANO LA KUPUNGUZA TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA, 4 DESEMBA, NEFALAND HOTEL DAR

                       mbunge Kikwete 

KAMPUNI ya TMS Consultants Ltd, inayojishughulisha na masuala ya ushauri wa biashara na uwekezaji nchini inatarajiwa kufanya kongamano la masuala ya Kilimo Hai [Organic Agriculture] tukio ambalo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete, 04 Desemba mwaka huu katika ukumbi wa hoteli ya Nefaland, Dar es Salaam.



Kwa mujibu wa taarifa kwa Umma iliyotolewa na Mwenyekiti wa kampuni ya TMS Consultants Ltd, Bw. Sebastian Kingu ameeleza kuwa, mbali na  kongamano hilo pia kutakuwa na maelezo kuhusu taratibu za kufuata ili kuweza kununua ploti za mashamba zilizopimwa kwenye Block Farms maeneo ya Vigwaza  Chalinze na Kiwangwa Bagamoyo, kwa mkopo usiokuwa na riba wala dhamana. Mtu anapomaliza kulipia mkopo wake, mchakato wa kupata hati miliki ya ploti ya shamba lake unaanza kufanyika.


"Hii ni kwa watu wote wanakaribishwa kushiriki kongamano na hakuna kiingilio ni bure na maji ya kunwa yatatolewa bure. Lengo tunataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kupata elimu na pia kuweza kuingia kwenye uwekezaji wa mashamba na kilimo hai…

'Karibu tuwekeze katika kilimo biashara tuongeze kipato na ajira kwa vijana'.


Aidha, alifafanua kuwa, Taasisi mbali mbali kama benki za NMB Bank Agribusiness Financing, NBC Bank Agribusiness financing, Jubilee Insurance Agribusiness insurance na Manufacture wa Organic Fertilizer na wengineo watakuwepo kuwasilisha mada kwa huduma zao za kilimo biashara hapa nchini.


Imeelezwa kuwa, mazao yatokanayo na kilimo hai yamekuwa na soko kubwa hapa nchini Tanzania, Afrika na duniani ambapo kilimo hicho kinatumia mbolea na madawa ambayo hayana madhara kwa binadamu na mazingira kinazingatia utunzaji wa mazingira kwa ajili ya manufaa kwa jamii, kiuchumi na kiafya.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI