Dar es Salaam tarehe 3 Desemba 2021- Kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za kidijitali, Tigo Tanzania, leo imekabidhi pikipiki moja na simu janja za kisasa kwa washindi wa wiki wa kampeni yake ya mwisho wa mwaka inayoitwa Wagiftishe - Gift Juu ya Gift, ambapo wateja wanatakiwa kununua ITEL T20 kwa bei ya 89,000/- kutoka duka lolote la Tigo nchini kote ili kupata nafasi ya kujishindia simu janja 504 na pikipiki 1 kila wiki kwa muda wa wiki 6.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alitangaza mshindi wa zawadi ya pikipiki wiki hii ambaye ni Noel Kabuje mjasiriamali kutoka Kurasini, Dar es Salaam, na washindi wa simu za kisasa kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania.
Akiwapongeza washindi, Shisael alisema, ‘Kama kinara wa soko katika mabadiliko ya mtindo wa maisha ya kidijitali nchini, Tigo sasa inahakikisha kuwa kila mtu anapata nafasi ya kumiliki simu bora ya kisasa kwa bei nafuu Zaidi kwa kila ununuzi wa simu za kisasa za ITEL T20 kutoka kwa maduka ya Tigo nchini kote, wateja waendelee kununua simu za ITEL T20 kutoka maduka ya Tigo nchini kote ili kuingia kwenye droo ya kupata nafasi ya kujishindia moja ya pikipiki 5 na simu janja ambazo bado zinawaniwa katika promosheni hiyo.’Shisael alieleza kuwa mteja anaponunua simu za kisasa aina ya ITEL T20 kutoka duka lolote la Tigo nchini kote, wafanyakazi wa huduma kwa wateja wa Tigo kwenye maduka ya Tigo hurekodi IMEI namba ya simu hiyo, jina la mteja na namba ya simu ya mkononi. Maelezo haya yameingizwa kwenye michoro ya kila wiki. Kila wiki Tigo inatoa zawadi ya pikipiki moja kwa muda wa wiki 6.
Kwa upande wake Noel Kabuje aliyejishindia pikipiki alieleza kufurahishwa kwake na zawadi hiyo akisema itamuwezesha kuanzisha biashara ya usafiri wa pikipiki (bodaboda).
‘Nimejiajiri pikipiki hii itanipa njia mbadala ya kujikimu kimaisha. Naishukuru sana Tigo kwa kujali wateja wake, si tu kwa kutoa simu za kisasa zenye ubora kwa bei nafuu, bali kuzioanisha hizi na zawadi zinazotoka ambazo sasa zitanisaidia kuboresha hali yangu ya kiuchumi,’ alimalizia Bwana Kabuje.
0 Comments