Header Ads Widget

UANZISHWAJI WA STASHAHADA ZA BIASHARA YA KILIMO NA TASNIA YA UBUNIFU WATAKIWA KUTOLEWA KWA VITENDO ZAIDI

 


Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali zanzibar bwana Ali Khamis Juma ameitaka Taasisi ya karume ya Sayansi na Teknolojia kuhakikisha kozi za uanzishwaji wa Stashahada za Biashara ya Kilimo na Tasnia ya Ubunifu ziwe zinatolewa kwa vitendo zaidi ili kutoa taaluma na ujuzi ulio bora kea jamii.


Ameyasema hayo wakati alipozungumza  katika mkutano wa kuwasilisha Mapendekezo ya Uanzishaji wa Stashahada za Biashara ya kilimo na Tasnia ya Ubunifu chini ya mradi wa Bear II,  huko katika ukumbi wa Wizara ya Elimu Mazizini Mjini Unguja.


Amesema hali hiyo itaweza pia kusaidia kuzalisha wataalamu waliobobea katika fani hizo na hivyo kuchagua ukuaji wa uchumi wa nchi.


Amesema ni vyema pia  kuandaliwe mafunzo mafupi ya fani hizo na ziwe za muda mfupi ili watu waweze kupata ujuzi zaidi utakaowawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi.


Hata hivyo amewashauri kozi za masoko na fani za vifungashio zipewe kipaumbile ili watu waweze  kuzalisha zaidi  na kujiendeleza kimaisha.


Nae Mkurugenzi wa Tasisi ya karume Dk Mahmoud Abdulwahab Alawi akiwasilisha mapendekezo ya Stashahada za Biashara ya kilimo na Tasnia ya Ubunifu amesema Taasisi hiyo ilikubaliwa kuandaa mitaala ya Biashara za Kilimo na Tasnia za ubunifu ikiwa na jumla ya programu nne.


Amezitaja Programu hizo kuwa ni pamoja na Usarifu wa mazao ya baharini, usarifu wa mazao ya matunda na mboga mboga, Teknolojia ya kazi za mbao pamoja na Miundombinu na maendeleo ya kidijitali.


Hata hivyo amesema malengo hasa ya mradi huo wa BEAR II, ni kuwapatia mafunzo wadau husika katika kujua fani  gani za kiujuzi zinahitaji tathmini  na matarajio, ikiwa ni pamoja na zinazohusiana na maendeleo vijijini, kilimo, utunzaji wa mazingira na mahitaji ya stadi isiyo rasmi.


Nao baadhi ya viongozi wa Wizara walioshiriki katika mkutano huo wameshauri kuingizwa fani ya kilimo cha kisayansi ili Wanafunzi wa wanaomaliza Elimu ya Sekondari ya Kilimo waweze kujiendeleza na fani hiyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI