Na Pamela Mollel,Monduli
Tamasha kubwa la uhuru bonanza linalotarajiwa kufanyika Wilayani Monduli siku ya Jumamosi wiki hii maandalizi yake yamekamilika kwa zaidi ya asilimia 90
Wakizungumza na waandishi wa habari waandaaji wa Bonanza hilo wakiongozwa na Mwenyekiti wao Costastine Shayo anasema tamasha hilo limeandaliwa na wadau wa michezo lenye lengo la kuibua vipaji pamoja na kusheherekea miaka 60 ya uhuru
Alisema kuwa mpaka sasa maandalizi ya bonanza hilo yamekamilika kwa zaidi ya asilimia 90 ambapo yameshirikisha chama cha soka na chama cha riadha
Katibu chama cha Mpira wa miguu Monduli Abubakary Hamis alisema kuwa kupitia bonanza hilo litaweza kuitangaza vyema wilaya hiyo
Hapo katika wilaya yetu ya Monduli kuna watu mashuhuri ambao walishatumikia taifa hili lakini pia tuna vivutio vingi"alisema Hamis
Aliongeza kuwa bonanza hilo litaleta chachu katika michezo hasa kwa upande wa wanawake ikizingatiwa wilaya hiyo ni jamii ya kifugaji
Msemaji wa Bonaza hilo Amir Mongi alisema kuwa zaidi ya wadau wa michezo 3000 wanatarajiwa kushiriki Mashindano haya ambayo yatashirikisha mpira wa miguu,riadha, mbio za baskeli ,netbol,pamoja na kukimbiza kuku
"Bonaza hili nilakukata na shoka nawaomba wadau wapenda michezo wajitokeze kwa wingi"alisema Mongi
0 Comments