Header Ads Widget

WAZAZI WATAKIWA KUACHA KUWAFICHA NDANI WATOTO WENYE ULEMAVU

 




Wazazi mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuacha tabia ya kuwaficha watoto hususani wenye ulemavu na badala yake wawapeleke mashuleni ili wapate elimu itakayosaidia katika maaisha yao ya baadae......Na Rehema Abraham


 Hayo yamesemwa na bi.Sofia Urio mkurugenzi wa kituo Cha kimontesory Cha kisane iliyopo Moshi mkoani Kilimanjaro wakati alipokuwa kwenye mahafali iliyofanyika shuleni hapo.


Aidha amesema kuwa kituo hicho kinatoa elimu kwa mfumo wa kimontesory ambayo inamsaidia wanafunzi kuelewa kwa haraka masomo wanayofundishwa.


"Kwa hiyo Kama mnavyoona watoto hawafundishwi kama wanavyofundishwa katika shele zingine ,wanajifunza wenyewe "


Hata hivyo akizungumzia mmomonyoko wa maadili kwa watoto, amesema kwa kiasi kikubwa wazazi wamekuwa wakichangia kumomonyoka kwa maadili ya watoto .



Akiwa mgeni rasmi katika mahafali hayo Sarafina Laban Mtangazaji wa redio kicheko live watoto wote wanapaswa kupatiwa elimu ili iweze kuwasaidia katika maisha Yao ya baadae.


Amesema kuwa Kuna changamoto ya wazazi kuwaficha watoto wenye ulemavu ndani na kutowapeleka mashuleni wakajifunze Mambo mbalimbali.


Sambamba na hayo amesema Kuna baadhi ya wazazi wanahitaji elimu ya saikolojia kwani wengi wao hawana uelewa wa faida anazopata mtoto anapopelekwa shuleni.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI