Na chausiku said, Mwanza
Rais wa Shirikisho Chama cha Riadha Tanzania Silas Isangi ameiomba serikali kuendelea kushika mkono mchezo huo kwani ndio unaoutambulisha nchi ya Tanzania.
Akizungumza mapema na Matukio Daima ameeleza kuwa mchezo wa riadha umeendelea kufanya vizuri Hapa nchini na nchi za ulaya na japani kwa sasa tofauti na kipindi cha nyuma.
"Tumejitahidi kuokoa huu mchezo ulikokuwa unaelekea shimoni mnakumbuka tulivyoingia madarakani tuliweza kuweka watu kambini kwa ajili ya mashinadano" alisema Isangi.
Isangi Ameeleza kuwa kwa sasa riadha imekuwa na mwamko mkubwa tofauti na zamani hivyo wamekuwa na mashindano mablimbali yaliyofanyika na kuweza kuibuka washindi.
" tulikuwa na mashindano ya rock city marathon ambapo watanzania walishika nafasi ya kwanza na wakenya wakafata nafasi ya pili hivyo tunafanya vizuri sana" alisema Isangi.
Ameeleza kuwa Kati ya michezo ya olympic iliyowezakufanyika japan walioweza kufuzu vigezo katika mashindano hayo ni riadha peke yake na kuweza kuitangaza Tanzania.
"Tuliposhiriki kwenye mashindano hayo tuliweza kujinyakulia ushindi wa nafasi ya saba (7) Duniani" Alisema Isangi.
Aidha ameeleza kuwa mbali na chamgamoto mbalimbali za kipesa katika maandalizi bado wanafanya vizuri katika mchezo huo.
Aidha ametoa wito kwa wazazi kuawaacha watoto kushiriki katika mchezo huo na kutowanyima ruhusa kwenda kufanya mazoezi ambapo michezo ni ajira.
" kwa mfano tulikuwa na mwana riadha wetu Alphonce Simbu alienda kukimbia Dubai marathon na amefanya vizuri kwa kushika nafasi ya pili Kwa masaa 2 na dakika 7 na sekunde 50" alisema Isangi
Kwa upande mwingine ameleeza kuwa kuanzia desemba hii kuanza mazoezi ya mashindano ya Samia Cup yatayofanyika jijini Dar -es- salam ili kuweza kuunda timu ya Taifa kwa mbio fupi na ndefu.
0 Comments