Nyuma ya mwaka 2009 serikali iliamua kuzipeleka shule zote za sekondari za hadhi ya ndogo TAMISEMI kwa nia moja ya kusimamiwa kwa karibu na mamlaka ya serikali za mitaa, kwani kulikuwa na ongezeko la shule za kata na ongezeko la wanafunzi kutoka MEMKWA na MESS. Kwani kwa wakati huo usimamizi wa shule hizi ulikuwa chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi....ADELADIUS MAKWEGA_DODOMA.
Lilikuwa ni jambo gumu Wizara ya Elimu yenye ofisi yake Dar es Salaam kuisimamia vizuri shule ya Kata Iliyopo Isimani Tarafani hivyo kuzipeleka shule hizo ziwe chini ya Tawala za Mikoa ilikuwa ni jambo la haki na la nia njema.
Tawala za Mikoa ndiyo walio jirani na watu mathalani uchangiaji wa nguvu kazi katika miradi kadhaa ya serikali wao ndiyo wanaosimamia kwa hiyo unapowashirikisha moja kwa moja wananchi wanatambua kuwa kwanza miradi hiyo ni mali yao na pili ushiriki huo hauna budi kuwa wakweli kwa manufaa ya jamii nzima..
Hivi karibuni Waziri Ummy Mwalimu amepiga marufuku kitendo cha kuwashusha vyeo walimu wakuu kwa visa vya shule zao kufanya vibaya. Akisema kuwa jambo hilo linapaswa kufanyiwa uchunguzi wakina kabla ya kufanyika hilo.
Swali ni je Waziri Ummy Mwalimu hawaamini Wakurugenzi Watendaji na Maafisa Elimu waliopo wilayani?. Je mheshimiwa huyu anayakumbuka maamuzi ya serikali ambayo maelekezo yake yalianza kutolewa tangu mwaka 2008 ya kuziondoa hasa shule za sekondari Wizara ya Elimu kwenda TAMISEMI wakati huo chini ya Mawazii Marehemu Brigedia Hassani Ngwilizi na Naibu wake Mizengo Pinda yalikuwa na lengo gani?
Nadhani Waziri Ummy anapaswa kuheshimu dhana ya shule hizo kuwa chini ya Wilaya husika. Mkuu wa watumishi serikalini wilayani ni Katibu Tawala yupo pia Mkurugeniz Mtendaji wote hao wakisimamiwa na Mkuu wa Wilaya wao wanotosha kuamua jambo kwa nia njema kuboresha elimu ya wilaya yao. Binafsi naona agizo hilo halina tija kwa jamii ya wapenda elimu wa taifa hili.Ninaandika haya siyo kuwa walimu wakuu waonewe la hasha, haki ni jambo la msingi lakini pia elimu yetu ni la msingi zaidi yayote.
Kuna kesi mojawapo ya shule ya sekondari moja mwalimu mkuu alikuwa ana mahusiano ya kimapenzi na mabinti watatu wa shule hiyo wa kidato cha nne. Jambo hilo lilikuwa la kawaida huku walimu wa chini nao wakiwa na wapenzi wao. Mwalimu huyu mkuu alikuwa na urafiki wa karibu sana na diwani wa kata hii ambaye alikuwa mtu mzima sana. Kwani mwalimu huyu alikuwa akimsaidia mno mheshimiwa diwani huyo kushinda uchaguzi kila mara.
Jambo hilo la mahusiano ya kimapenzi baina ya walimu na wanafunzi lilimkwaza mno Matroni wa shule hiyo ambaye na yeye alikuwa mwalimu pia.
Mama huyu alibaini kuwa hali hii ni mbaya na ina athari kwa shule na elimu ya watoto hawa wa kike. Mwalimu ambaye ni Matron alitoa taarifa kwa Mkurugenzi Mtendaji juu ya shida hiyo na siku hiyo Mkurugenzi alifanya uchunguzi wa suala hilo na wanafunzi waliwataja walimu ambao walikuwa na mahusiano na wanafunzi wa kike kwa kuwataja kwa siri katika karatasi maalumu.
Shule hii haikuwa ikifanya vizuri kabisa na wala hakukuwa na mikakati yoyote ya kupambana hali hiyo. Mwalimu huyu alipokuwa akiguswa diwani alikuwa akiyatazama maslahi yake ya kisiasa tu. Je hapo kuna haja ya kumngoja Katibu Tawala wa Mkoa na Waziri Ummy?
Tamati ya yote mwalimu Matron alisumbuliwa sana kwani baada ya yule Mkurugenzi Mtendaji kuhamishiwa, huku akipata misukosuko kadhaa kwa nia yakea njema ya kumlinda mtoto wa kike.
Shule hizi zimebeba watoto wa watu ambao jukumu ni kuwaanda kuwa wazazi wa taifa la kesho, kuwa walimu wakesho, kuwa wauguzi wa kesho na kuwa raia wema wa Tanzania ijayo, ukisema unamsubiri Afisa Elimu wa Mkoa, au Katibu Tawala hilo ni kosa kubwa, wale wanaotoa matamko hayo ukifuatilia hawana watoto wao katika shule hizi za kata, huku wakitaka watoto wao kufundishwa na walimu wazuri katika shule hizo bora.
Viongozi hawapaswi kugombania nafasi zao kinachopaswa kugombaniwa kile wanachotakiwa kupatiwa jamii ambacho ni elimu bora.
Suala na kusema kuwa hakuna .mkuu wa shule atakayeondolewa kwa kushushwa cheo kama shule yake haitofanya vizuri kwa kutamkwa na Waziri wa TAMISENI maana yake ni kuwa watoto kutofanya vizuri kwake si tatizo. Watanganyika walidai uhuru ili waweze kuwa na elimu bora, wasome vizuri ili waweze kushindana na vizazi vya mataifa mengine.
Walimu wakuu kulingana na waraka nambari 3, 2016 wa elimu bure wamepewa majukumu mengi likiwamo la kushirikiana na wazazi na bodi/kamati kutatua changamoto mbalimbali za shule zao huku wakifuata taratibu.
Utaratibu wa kupambana na ujinga ni vita kama vilivyo vita vingine, kusema kuwa walimu wakuu wanoafanya vibaya wasiondolewa ni udhaifu mkubwa ambao unapaswa kupingwa. Huku waheshimiwa hawa kujikita kutenga pesa za kutosha kwa shule zetu kutatua uhaba wa walimu na gharama za ulinzi wa shule zetu.
Kwa mfano uliohai shule nyingi nchini Tanzania kwa sasa kuna changamoto ya malipo ya fedha za ulinzi, hakuna utaratibu mzuri wa jambo hili. Hapo awali chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi walinzi wengi walikuwa na ajira za kudumu lakini suala hlo lipo chini ya serikali za vijiji/mitaa kwa sasa jambo hili linalalamikiwa mno.
Wizara ya Elimu na TAMISEMI wana wajibu wa kutambua kuwa ushirikishwaji wa jamii hana budi, watake na wasitake kwani ndivyo ilivyokuwa tangu vijiji vya ujamaa.
Mathalani hivi sasa kuna shule zimepatiwa fedha za UVIKO 19 baadhi ni milioni 20 wakiambiwa kuwa fedha hizo zijengwe darasa moja tangu mwanzo hadi mwisho bila ya kuhitaji nguvu za wananchi.
Sawa ni jambo zuri lakini katika baadhi ya maeneo milioni 20 inaweza kujenga madarasa mawili kama wananchi watachangia nguvu zao ikiwamo tofari, mawe na mchanga.Shida si kuwa na darasa moja zuri na kusema darasa hili kalijenga fulani bali shida ni kuwa madarasa ambayo yataisaidia wanafunzi wetu kuweza kusoma.
Suala siyo kuwa na elimu inayotamkwa kuwa ni ya bure wakati kiukweli bado hatujafikia kiwango hicho. Suala la elimu bure tuliache katika kumbukumbu tu tu maisha ya Julius Nyerere ndiye aliyeweza kuitoa kweli hiyo elimu bure.Kwa leo ninaishia hapo. Nasema siku nyengine.
makwadeladius@gmail.com
0717649257
0 Comments