Header Ads Widget

HALMASHAURI YA KIBAHA YAPANDA MITI 200 LENGO LIKIWA NI KUINUSURU DUNIA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

 


Halmashauri ya Mji Kibaha imeanza maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania kwa kupanda miti 200 kwenye shule ya sekondari picha ya Ndege ikiwa ni kuunga mkono Juhudi za kuinusuru dunia na uharibifu wa Mazingira.


Zoezi hilo limefanyika Kihalmashauri kwenye kata ya Picha ya Ndege likiongozwa na Anatory Mhango aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Sara Msafiri.


Mhango ametoa rai kwa Wilaya zingine kupanda miti kwa wingi hasa wakati huu wa Mvua ili kuifanya Tanzania kuwa ya kijani.


Diwani wa Kata mwenyeji Mhe.Karimu Mtambo amesema upandaji miti ni jambo lisilokwepeka kwani huzalisha hewa ya oksijeni ambayo ni muhimu Sana kwa maisha ya binadamu 


William Msemo Afisa Misitu wa Halmashauri amesema Kibaha Mji inatarajia kupanda miti 10,500 ifikapo Juni mwaka,2022 ilihali kwenye shule ya Picha ya Ndege pekee tayari kumeshapandwa miti 1200,ikiwemo 20 ya Matunda.


Zoezi hilo lilihudhuriwa pia na Kaimu Mkurugenzi  George Mbogo,Wakuu wa Idara,Vitengo na watumishi wengine.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI