Viongozi wa Chama Cha mapinduzi mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuhakikisha kuwa wanatenda haki ,ikiwa ni pamoja na kuwachia wanachama wachague Kiongozi wanaomtaka ...........Na Rehema Abraham.
Wito huo umetolewa na Katibu wa Chama Cha mapinduzi CCM wilaya ya Siha wakati alipokuwa katika semini na viongozi wa Chama iliyofanyika wilayani hapo.
Aidha amesema kuwa katika Semina hiyo wamewaasa viongozi hao kuhakikisha kuwa hawatembei na wagombea mfukoni na vikao vya uchujaji wa viongozi vitende haki inayostahili kwa wote.
Amesema kuwa Kama Kiongozi yeyote atabainika kupokea rushwa ili ampitishe Kiongozi Sheria itachukua mkono kwani katiba ya Chama hairuhusu Kiongozi yeyote kupokea rushwa.
Akiwa mgeni rasmi katika mafunzo hayo Solomon Itunda Katibu Mkuu msaidizi idara ya oganaization Ccm Taifa, amesema kuwa wameamua kutumia mafunzo hayo kuongeza hamasa kwa Chama ili zoezi hilo liende kwa kasi .
Amesema wameamua kuwatumia viongozi wa ngazi za chini ambao wao ndio Wana wanachama ili waweze kuhakikisha kuwa ifikapo 2021 wanachama wote wawe wamesajiliwa kwa njia ya kielectonic.
0 Comments