Header Ads Widget

BODI/KAMATI ZA SHULE ZINAVYOOKOA JAHAZI LA SODO

 




Siku ya leo nikiwa Uwanja wa BenjaminI Mkapa nilitumiwa ujumbe na kupigia simu kadhaa na ndugu zangu waliosoma makala yangu juu ya Chuki na Mwalimu wa Kichaga katika baadhi ya maswali yao walitaka kujua kwa kina namna wazazi/walezi wanavyojipanga na kuwalinda mabinti zao pale wanapotokea na tukio ukuaji kwa mabinti wakiwa katika mazingira ya shule.............NA ADELADIUS MAKWEGA _UWJ-BENJAMINI MKAPA.


Maswali hayo yalikuwa mengi huku nikiwa vigumu kuweza kuyajibu maswali haya yote niliona ni busara kama nitayajibu maswali haya katika mtindo wa makala pia.


Kwa mujibu wa uendeshaji wa shule za msingi/ sekondari za umma na binafsi nchini Tanzania kila shule inatakiwa kuwa na kamati ya shule kwa mujibu wa Waraka wa Elimu nambari 4 wa mwaka 2016 kamati ya shule huwa na wajumbe 13 ambapo wajumbe 5 ni miongoni mwa wazazi /walezi wenye watoto shuleni waliochaguliwa miongoni mwa na wazazi/ walezi wenyewe.


Mwenyekiti lazima awe ni mzazi au mlezi anayeishi jirani na shule hiyo na awe na elimu kuanzia kidato cha nne, makamu mwenyekiti awe na sifa kama za mwenyekiti, katibu awe mwalimu mkuu wa shule, wajumbe wawili kutoka serikali ya mtaa/kijiji shule ilipo, mwalimu wa taaluma katika shule hiyo, mwalimu mmoja anayechaguliwa na walimu wenzake kutoka stafu ya shule hiyo mara nyingi huwa kiongozi wa chama cha walimu(CWT/CHAKAMWATA) na afisa elimu wa kata husika.


Kamati/Bodi ya shule pia huwa na kamati ndogo ndogo  tano nazo ni kamati ya mipango na fedha, kamati ya miundombinu na mazingira, Kamati ya taaluma na nidhamu, kamati ya malezi na ushauri nasaha na kamati ya Afya na chakula.


Makala yangu ya Chuki na mwalimu wa Kichaga inaangukia kamati mbili za shule nazo ni kamati ya afya na chakula na kamati ya malezi na ushauri nasaha. Kamati ya afya na chakula ina majukumu manne hapa mimi nitalitazama jukumu ya moja tu la kupatikana kwa huduma ya kwanza ambayo ni kupatikana dawa za dharura na kwa sodo.


Ukija katika kamati ya malezi na ushauri nasaha hapa ina kazi sita lakini mimi nitatazama kazi mbili tu nazo moja wanafunzi wanapatiwa na kutengewa chumba maalumu cha ushauri na unasihii pili wanapata huduma ya ushauri na unasihi.


Sasa hapa kinachofanywa na kamati hizo mbili wanatazama uwezo wa shule na rasimali zao.


Kamati hizo huwa makini mno kwa kuwachagua akina mama wenye nyumba jirani na shule, walimu wa kike wenye makazi jirani na shule na wakati mwingine hata wafanyabiashara ndongo jirani na shule kuokoa jahazi linapotokea tukio tukio lolote linalomuhusu binti.


“Mama X naomba uwe unamuangalia binti yangu maana naona umri wake umekaribia, maana aibu yako ni aibu yangu, tusaidiane, kwangu ni mbali.” Haya ni maneno ya kawaida sana kwa akina mama wakiongea na ndugu zao waliojirani na shule.


Katika hali kama hizo wazazi wengine katika kamati hizo wanachangishana na kupatikana vifaa vya kuwahudumia watoto wa kike zikiwamo sodo za dharura ambazo mara zote hazilingani na mahitaji halisi.


Kamati hizi huwa makini huku wakiwa na kiongozi mwanafunzi katika kila darasa ambaye amepevuka na anauelewa wa mambo haya kuwasimamia na kuwaelekeza pa kwenda mara baada ya hali hiyo ya dharura inapotokea katika mazingira ya shule.


Ndiyo maana msisitizo unapaswa kufanya kwa kuwezesha shule kuwa na sodo za kutosha na huduma zingine za afya za uzazi kwa wanafunzi shuleni ilikusaidia mabinti zetu waweze kusoma kwa bidii.


Labda kwa kuhitimisha ni jambo la msingi na umuhimu mkubwa kwa wazazi wenye watoto kushiriki vikao vya shule ilimkumsaidia mzazi kutambua mambo mengi ya malezi ya mtoto wake. Shida iliyopo ni kwa shule zetu za umma lakini shule za kulipia hilo siyo tatizo na ndiyo maana hata waraka wa Elimu nambari 3, 2016 umezitaja baadhi ya shule za kulipia za umma ambazo haziguswi na waraka huu ambazo ni Shule ya Msingi Tanga, Shule ya Msingi Lupilisi (Ruvuma),Shule ya Msingi Nuru(Mbeya), Shule ya Msingi Angaza(Mbeya), Shule ya Msingi Iringa(Iringa), Shule ya Msingi Oysterbay (Dar es Salaam), Shule ya Msingi Diamond(Dar es Salaam),Shule ya Msingi Olympio (Dar es Salaam), Shule ya Msingi Kisimani (Arusha), Shule ya Msingi Arusha (Arusha).


Ndiyo maana bado ninalipigia chapuo suala la kupatikana sodo la kutosha za bure katika kila shule na kuwapatia mabinti wahitaji sodo  hizo huku kukiwa na chumba maalumu cha huduma hizo. Silisemi hilo kwa kuwa sasa kuna Rais mwanamke tu bali hata viongozi wanaume wa taifa letu kama Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Philip Mpango anazaliwa na mwanamke, ana ndugu zake wanawake na ana watoto wakike. Hilo ni jukumu letu sote. Naweka kalamu yangu chini nikiwa haba Benjamini Mkapa nikiendelea na lile lililonileta hapa. Nasema  siku nyengine.


makwadeladius@gmail.com

0717649257

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI