Sheria Ardhi Namba 4 na Sheria ya Ardhi ya Kijiji Namba 5 zote za mwaka 1999 zinaainisha vyombo vya utatuzi wa migogoro ya ardhi kuanzia ngazi ya kijiji hadi taifa ambavyo uundwaji wake unaainishwa katika Sheria ya Mabaraza na Mahakama za Ardhi Namba 2 ya mwaka 2002. Mamlaka inayosimamia mabaraza ya ardhi ya vijiji na mabaraza ya kata ni naibu msajili wa vijiji na ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya husika.
Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya yanasimamiwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa zinasimamiwa na Wizara ya Katiba na Sheria. Mamlaka zote hizi zina wajibu wa kuandaa makadirio na matumizi ya vyombo wanavyovisimamia kwa mujibu wa sheria. Sheria ya Mabaraza na Mahakama za Ardhi Namba 2 ya mwaka 2002 inaainisha vyombo vya utatuzi wa migogoro kama ifuatavyo:
Baraza la Ardhi la Kijiji ni chombo cha usuluhishi wa migogoro ya ardhi ndani ya kijiji kwa kutumia taratibu za mila na desturi za eneo husika. Baraza la Ardhi la Kijiji linaundwa na wajumbe 7 ambao 3 kati yao watakuwa wanawake. Wajumbe hawa watateuliwa na Halmashauri ya Kijiji na kuafikiwa na Mkutano Mkuu wa Kijiji.
Sifa za Wajumbe wa Baraza la Ardhi la Kijiji kwanza awe na sifa nzuri na heshima kijijini kama mtu mwenye msimamo na mwenye kufahamu sheria za kimila za ardhi. Pili awe hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa la jinai, pia kwakukosa uaminifu au kukosa maadili. Tatu awe raia wa Tanzania, Nne. awe mkazi mwenyeji wa kijiji, Tano awe mwenye akili timamu na;Sita awe aliyetimiza umri wa miaka 18. Saba asiwe ni mbunge. Nane asiwe hakimu mwenye mamlaka kwenye Wilaya ambayo ndimo limo baraza.
Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi Tanzania kwanza asiwe mjumbe wa Halmashauri ya Kijiji. Mtu yeyote anayekosa moja ya sifa zilizotajwa hapo juu kwa mujibu wa sheria hawezi kuwa mjumbe wa baraza la ardhi la kijiji. iii. Ukomo wa wajumbe wa Baraza la Ardhi la Kijiji Kila mjumbe atatumikia kwa kipindi cha miaka 3 lakini anaweza kuteuliwa tena kwa kuzingatia taratibu zile zile za awali, isipokuwa tu pale ambapo Mjumbe alijiuzulu mapema, kufariki au atakosa sifa tajwa hapo juu.
Majukumu ya Baraza la Ardhi la Kijiji ni pamoja na kupokea malalamiko yanayohusu ardhi kutoka kwa wanakijiji, kuitisha vikao vya kusikiliza madai ya migogoro kutoka kwa walalamikaji na kusuluhisha migogoro ya ardhi iliyoletwa mbele yake kwa lengo la kufikia maridhiano baina ya wahusika.
Vikao katika Baraza la Ardhi la Kijiji Kikao cha baraza kitakuwa na wajumbe 7 hata hivyo kikao kinaweza kufanyika kikiwa na wajumbe wa 4 ambao kati yao 2 lazima wawe wanawake. Baraza litamteua mmoja wa wajumbe kuwa mwenyekiti na mwingine kuwa mtunza kumbukumbu za baraza. Endapo mwenyekiti na mtunza kumbukumbu hawapo wajumbe watakaouhudhuria kikao watamteua mmoja wao kuendesha kikao.
Mambo ya kuzingatiwa wakati wa suluhu ni mambo makuu matatu Kuzingatia, kwanza misingi yoyote ya mila na desturi za eneo husika.Pili kuzingatia haki za asili za watu Kama mila na desturi hazitoshelezi. Tatu kuzingatia njia mbadala za utatuzi; kama vile uzoefu wa kutoa suluhu, hekima na busara. Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji, kwa mujibu wa sheria ni vyombo vya kutoa suluhu tu, hayana mamlaka ya kutoa hukumu. Ingawa uzoefu unaonesha vyombo hivi ama kwa kutokujua au kwa kujua vimekuwa vikitoa hukumu, kutoza faini na kupokea fedha za kufungulia mashauri kutoka kwa wananchi kinyume kabisa na matakwa ya sheria.
Vyombo hivi havina budi kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria, hasa kujaribu kutumia zaidi mila na desturi za sehemu husika kwa lengo la kusaidia wazalishaji wadogo kupunguza migogoro ya ardhi na kuvifanya vyombo hivyo kuwa kimbilio la wanyonge.
Hakuna utaratibu wa kukata rufaa kutoka Baraza la Ardhi la Kijiji kwenda Baraza la Kata kama mwananchi hakuridhia suluhu iliyofikiwa. Kwa maana hiyo mwananchi yeyote ambaye hakuridhia suluhu kijijini basi anaruhusiwa kwenda Baraza la Kata kwenda kufungua shauri Lake. Sheria Namba 5 ya Ardhi ya Kijiji ya 1999 na Sheria ya Mabaraza na Mahakama za Ardhi Namba 2 ya 2002, zinayatambua mabaraza ya ardhi ya vijiji kama vyombo vya utatuzi wa migogoro ya ardhi kwa njia ya suluhu tu na siyo kutoa hukumu.
Kwa kuhitimisha hapa ifahamike wazi kuwa kijiji kwa sehemu kubwa ndicho chenye ardhi hawa ndiyo wanaofahamu vizuri mipaka yote ya eneo hilo huku ikiwatambua na wakaazi wa asili wa eneo hilo, kwa hiyo kama baraza hili linatumika ipasavyo lazima litafanya uamuzi wa haki, pia uamuzi salama wa mgogoro huo. Kwa sababu kila kijiji kina shughuli yake ya msingi iliyotajwa wakati wa usajiri iwe kilimo au ufugaji na ndiyo maana taasisi kama MVIWATA zimekuwa zikitoe elimu hiyo ya wakulima wadogo wadogo kukwepa madhara yanayoweza kutokea panapotokea migogoro.
makweadeladius@gmail.com
0717649257
0 Comments