Header Ads Widget

TRUMP ASEMA MAKOMBORA YA PATRIOT TAYARI YAMETUMWA UKRAINE

 

Rais wa Marekani Donald Trump alisema Jumanne, bila kutoa maelezo, kwamba makombora ya Patriot tayari yalikuwa yametumwa Ukraine chini ya utaratibu mpya wa utoaji.

"Tayari wametumwa," Trump alimkatiza mwandishi wa habari ambaye alikuwa ameanza kuuliza swali juu ya makombora ya Patriot.

"Yanatoka Ujerumani na Ujerumani itayabadilisha. Na katika hali zote, Marekani italipwa kikamilifu. Kwa hivyo kinachotokea ni, unajua, kimsingi ni Umoja wa Ulaya unayatoa, lakini wacha tuseme kwa njia ya NATO, ni sawa sana, lakini NATO itatulipa kwa kila kitu. Katika baadhi ya matukio, tutalipwa moja kwa moja na nchi za Umoja wa Ulaya," Trump aliendelea.

Alipoulizwa ikiwa vikwazo vya pili kwa nchi zinazonunua mafuta ya Urusi vitawaumiza watumiaji wa Amerika, Trump alisema: "Sidhani hivyo. Nadhani jambo hili lote litaisha mwishowe. Linapaswa kuondolewa. Na Putin anasema, 'Nataka amani, nataka amani,' lakini bado hajafanya kile anachosema. Kwa hivyo nadhani litaondolewa. Lakini tutaona."

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI