Header Ads Widget

WHO YAKANUSHA TAARIFA YA DAWA YA KUTIBU UVIKO -19:KUGUNDULIKA


Na Francis Godwin, Matukio Daima Media

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema hadi sasa hakuna dawa yoyote iliyoguliwa kutibu  ugonjwa wa Corona (Uviko-19), licha ya kuwepo kwa baadhi ya dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini.

Septemba mwaka huu, WHO iliidhinisha matumizi ya dawa ya Regeneron kwa ajili ya kutibu watu wenye dalili kali za ugonjwa wa Corona (Uviko-19) na hawana kinga ya kutosha mwilini.

Dawa hiyo ambayo ni mchanganyiko wa dawa aina ya Casirivimab na Imdevimab inapendekezwa kutumika kwa wagonjwa ambao si wagonjwa mahututi lakini wako katika hatari ya kuweza kulazwa hospitalini kutokana na Uviko-19.

Hata hivyo, baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakipotosha kuwa dawa ya Uviko-19 imepatikana na watu hawana haja ya kupata chanjo.

Katika mtandao wa Facebook, baadhi ya watu wanadai dawa aina ya “Ivermectine” inatibu Uviko-19, jambo ambalo siyo sahihi.

 



Dawa hiyo ni kweli inatibu Uviko-19?

Dawa ya ‘Ivermectine’ haijaidhinishwa kutibu Uviko-19. Dawa hiyo hupewa wagonjwa wanaosumbuliwa na minyoo na maumivu ya tumbo yanayotokana na vimelea hivyo, kwa mujibu wa tovuti ya masuala ya afya ya WebMD. 

Hata WHO imekanusha kuhusu dawa hiyo kutibu Uviko-19 na kuwataka watu kupata taarifa sahihi za ugonjwa huo kupitia vyanzo sahihi na si vinginevyo. 

Pia WHO inaendelea kusisitiza watu kujikingana na ugonjwa huo kwa kuvaa barakoa, kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima, kunawa mikono kwa maji tiririka na vitakasa mikono.

Njia nyingine ya uhakika kujikinga na maradhi hayo yanayoitesa dunia kwa sasa ni kuchanja chanjo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI