Header Ads Widget

VUNJABEI WAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO VYA TSH MILIONI 24 LIPULI FC

kampuni ya Vunja Bei imekabidhi Kwa mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Moyo Vifaa vya michezo vyenye thamani ya Tsh Milioni 24 Kwa ajili ya timu ya Lipuli Fc ya mkoa wa Iringa

KAMPUNI ya Vunja Bei imekabidhi Vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi Milioni 24 Kwa timu Lipuli Fc inayocheza ligi daraja la pili .


Vunja Bei  kama wadhamini wa timu hiyo wamekabidhi Vifaa hivyo Leo mbele ya mkuu wa wilaya ya  Iringa Mohamed Moyo na Viongozi wa Lipuli Fc .

Akipokea vifaa hivyo Moyo alipomgeza  uongozi wa kampuni ya Vunja bei kwa upendo wao waliouonyesha kwa timu ya Lipuli na kuwaomba wengine pia wajitokeze katika kudhamini timu hiyo ili iweze kupanda daraja na hatimaye kucheza ligi kuu.

''Niwashukuru vunjabei kwa kuleta vifaa hivi, pia nitoe shukrani kwa uongozi wao kwa kutimiza ahadi waliyokuwa wameiweka maana sio kampuni zote zinaweza kutimiza kile ambacho watakuwa wamekiahidi ila nyinyi mmeweza na ukiangalia timu hii imeshuka daraja kwa sasa, hivyo naomba muendee na moyo huohuo wa kuisaidia timu hii'' alisema Moyo

Kuwa msaada huo ni mkubwa na unaongeza nguvu Kwa timu ya Lipuli Fc 

"Sisi kama serikali tunafanya kazi na sio kila siku utatokeza hadharani na kusema mimi naisaidia timu timu ya lipuli ina heshima kubwa kwa iringa hivyo lazima swala la wadhamini tulifanyie kazi"

Alisema timu ina  changamoto nyingi hivyo kama serikali kwa kushirikiana na wadau wengine tutazifanyia kazi na tutazungumza na uongozi pamoja na wale waliokuwa wanaisimamia kipindi ipo kwenye ligi warudi kuisapoti tena

"wadau vunja bei ameanza kwahiyo na nyinyi wengine roho zenu zikae sawa ili tuisaidie lipuli halafu hizo changamoto nyingine tutazitatua, kampuni ni nyingi sana hazitaki kuwekeza kwenye michezo ila tutaongea nazo tune watatusaidiaje"

Kwa upande wake Fadhili alisema Vunja Bei wamekuwa wadhamini wa timu hiyo Kwa miaka kadhaa  ambapo mwaka jana walitoa vifaa na mwaka huu wanatoa vifaa vyote vya timu ya Lipuli kwa ajili ya kuchezea uwanjani na mazoezi.


"Mungu akipenda huko mbele tutafanya vizuri zaidi lakini kwa sasa tumetoa vifaa visivyopungua tsh milioni 24 pamoja na fedha kidogo "


Alisema kuwa Vunja Bei imetoa vifaa tu ila kwa wale wenye uwezo wa kuisaidia Lpuli kwa namna yeyote ili iweze kurudi kwenye ligi kuu watakuwa wameisaidia sana timu

"kuanzia leo jezi za timu ya lipuli zitauzwa katika maduka ya vunja bei hivyo wakazi wa iringa wametakiwa kujitokeza kwa wingi kununua jezi kwa ajili ya kuijenga timu maana ndio timu ya kuiletea furaha wana Iringa" 

ni sehemu ya mkataba ambao tulisaini na timu ya lipuli mwaka jana na kukubaliana kuwakabidhi vifaa hivi kwa muda wa miaka miwili, mwaka huu ndio mkataba unaisha Mungu akipenda tutasaini mkataba huu kwa miaka mingine kwa ajili ya kukabidhi vifaa kwa miaka ijayo.


Kwa upande wake mwenyekiti wa muda wa Lipuli Fc Mussa Wanguvu alipongeza msaada huo na kuomba wadau wengine kuunga mkono jitihada za Vunja Bei 

























 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI