Waziri Aweso aliushukuru uongozi wa Benki ya Exim India kwa kusafiri kuja nchini mahsusi kwa kukutana na Serikali ili kuona utekelezaji wa mradi huo unaanza, na kusema mpango wa Serikali ni kuhakikisha huduma ya majisafi inafika asilimia 95 katika maeneo ya mijini na asilimia 85 vijijini.
Waziri aliwataka Benki ya Exim kuhakikisha wanatoa kibali haraka ili mikataba ya ujenzi wa mradi wa miji 28 inasainiwa kwa sababu kibali hicho kimechelewa kutolewa kwa muda mrefu.
Alisema India ni moja ya washirika wakubwa wa Sekta ya Maji na kielelezo ni mradi mkubwa wa maji wa Tabora-Igunga-Nzega uliokamilika kwa kiasi cha shilingi bilioni 600, na wananchi zaidi ya milioni 1.2 wanapata huduma ya majisafi, salama na yenye kutosheleza.
Aweso aliainisha kuwa Wizara ya Maji sio kikwazo katika kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata huduma ya maji, na lengo la Serikali ni kumtua mama ndoo kichwani katika kona zote za nchi.
Akiongea katika kikao hicho, Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) alisema wanufaika wa mradi huo wanasubiri kuona kazi inaanza na viongozi wamejipanga kuratibu kazi mbalimbali za utekelezaji wa mradi huo.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga alisema japo mradi huo umechukua muda kuanza kupitia vikao hivi vinavyofanyika hivi sasa matarajio ya kuanza kwa mradi huo ni makubwa.
Ujumbe wa Benki ya Exim India uliongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo Bw. Gaurav Bhandari aliyesema uhusiano kati ya India na Tanzania ni mkubwa na wa siku nyingi, na kuahidi kampuni bora zitatumika katika utekelezaji wa miradi mbalimbali hapa nchini.
Mradi wa maji wa miji 28 umepangiwa kiasi cha Dola za Marekani milioni 500 ikiwa ni zaidi ya shilingi trilioni moja ambazo ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya India kupitia Benki ya Exim India.

0 Comments