Header Ads Widget

MAKUMBUSHO YA JIOPAKI (URITHI GEO MUSEUM) NI KISIMA CHA ELIMU: WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR



Na Emmanuel Saitoti, Karatu.

Wahadhiri na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) tarehe 21 Novemba, 2025 wamefanya ziara maalumu ya mafunzo katika Makumbusho ya Jiopaki ya Ngorongoro Lengai iliyopo Karatu Mkoani Arusha ili kuongeza uelewa wa wanafunzi kuhusu masuala ya  akiolojia, utamaduni, Jiografia, jiolojia pamoja na  historia ya sayansi na mazingira.

Wakiwa katika makumbusho hiyo wanafunzi walikutana na wataalam wa fani mbalimbali na kupata elimu kuhusu jiopaki ya Ngorongoro, elimu ya miamba,   sayansi na mazingira, tamaduni za makabila yaliyopo jirani na hifadhi ya Ngorongoro pamoja na vivutio vinavyopatikana katika hifadhi hiyo.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha SUZA na mkuu wa Msafara huo Dkt. Abdallah Mkumbukwa amesema ziara hiyo ni darasa kubwa kwa wanafunzi wa SUZA hasa kuunganisha masomo waliyosoma kwa nadharia kuwa ya vitendo kwa uhalisia wa kisayansi na kimazingira na kuita makumbusho hiyo kuwa ni kisima cha elimu ya miamba, jiolojia na utamaduni.

 



Msimamizi wa Makumbusho ya Jiopaki ya Ngorongoro Lengai, Afisa Uhifadhi Mkuu Dkt. Agness Gidna amesema tangu makumbusho hiyo kufunguliwa mwezi Oktoba, 2025 imeendelea kuvutia wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ambao wanakuja kutalii na kujifunza masuala ya Jiolojia, akiolojia na urithi wa utamaduni wa makabila mbalimbali kupitia maonesho na taarifa zilizowekwa katika Makumbusho hiyo.

“Tumepata maarifa mengi mapya na ya kisasa kupitia makumbusho ya jiopaki ya Ngorongoro Lengai, wanafunzi wetu wameelimika masuala mbalimbali kuhusu muonekano wa dunia kwa miaka mingi iliyopita na ilivyo sasa, maumbile asilia yanayopatikana katika ukanda wa bonde la ufa, mwamba wenye umri wa miaka milioni tatu iliyopita unaopatikana hifadhi ya Jiolojia ya Ngorongoro-Lengai na tamaduni za makabila ya Wahadzabe, Wairaqw, Wadatoga na Wamasai ambayo yote unayapata hapa" aliongeza Dkt. Mkumbukwa.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI