Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB) Mkoa wa Mtwara imepokea malalamiko 72 huku malalamiko 35 yakihusishwa na rushwa huku malalamika 37 hayakuhusu rushwa. mwandishi wa matukio daima Florence Sanawa anasimulia kutokea Mtwara
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Mtwara Enock Ngailo alisema kuwa katika malalmiko hayo 35 yalifanywa uchunguzi ili kudhibitisha makosa ya rushwa na uchunguzi wake bado unaendelea.
Alisema kuwa katika malalamiko 37 ambayo hayakuhusu rushwa matano yalishauriwa kuhamishiwa katika idara zingine kwa ufuatiliaji zaidi.
Ngailo alisema kuwa taasisi zinazolalamikiwa ni halmashauri zinaongoza kwa makosa 33, Vyama vya ushirika 14, maji 3 polisi 3 benki 2 mahakama 1 bima 1 tanesco 1 tanroad 1 na sekta binafsi 1.
Katika kipindi cha kuanzia Julai mwaka huu hadi Septemba walifatilia matumizi ya fedha za umma katika utelekezaji wa miradi ya maendeleo, ambapo baada ya uchunguzi huo ilibanika kuwepo kwa mianya ya rushwa ambayo imefanyiwa kazi katika vikao vya wadau na kutoa elimu kwa lengo la kuimarisha usimamizi wa miradi hiyo.
0 Comments