Header Ads Widget

MAHAKAMA YA MWANZO YAANZISHWA THEMI ARUSHA

Kutokana na idadi ya watu  kuongezeka na kupelekea mahakama ya mwanzo ya Arusha kuwa na msongamano wa mashauri kumepelekea kuanzishwa kwa mahakama ya mwanzo Themi ili wananchi weweze kupata huduma iliyobora. mwandishi wa matukio daima Teddy Kilanga anaripoti kutokea Arusha

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mahakama ya Themi,Jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Arusha, Moses Mzuna alisema uwepo wa mahakama ya mwanzo  hiyo kunafanya jiji la Arusha kuwa na mahakama mbili kwani hapo mwanzo kulikuwepo mahakama ya mwanzo ya Maromboso pekee yake.

Alisema kuwepo kwa mahakama mbili katika jiji ya Arusha kutasaidia kupunguza  msongamano wa mashauri uliokuwepo awali kwa Maromboso kwani yawezekana tatizo la msongamano wa wadaawa wenye kesi wamelipunguza lakini bado utakuwepo kwa mahabusu na wafungwa gerezani likaendelea kutokana na wilaya karibu zote za mkoa wa Arusha hutegemea gereza moja la Kisongo.

"Nadhani ni wakati mwafaka kila wilaya kuwa na gereza lake kwani msongamano mwingine huchangiwa na utaratibu wa kesi karibia zote kuwakamata washukiwa kabla ya kukamilisha upelelezi na imekuwa kwa makosa ya kawaida ya jinai isipokuwa mauaji washukiwa wapewe dhamana polisi,"alisema Jaji Mzuna.

Jaji Mzuna alisema ni vyema washukiwa wakapelekwa mahakamani tu baada ya kukamilika kwa upelelezi na hatimaye kesi kuanza kusikilizwa  mara moja hivyo ni imani yake wadau wa haki jinai watalifanyia kazi ili sheria itungwe mahsusi katika hilo kwa kurekebisha sheria ya mwenendo wa makosa jinai(CPA).

Sambamba na hilo Jaji Mzuna alisema jana Novemba 2,2021 wanahamia katika jengo la mahakama jumuishi lililozinduliwa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania ,Samia Suluhu Hassan mnamo Oktoba 6,2021 kwani uwepo wa majengo hayo utasaidia kurahisisha utendaji kazi kutokana na mahakama zote kuanzia ya watoto, mwanzo, wilaya, mkoa ,mahakama kuu, Masijala ndogo ya mahakama  ya rufani vyote vinakuwepo.

"Uwepo wa mahakama zote utasaidia kupunguza gharama za usafiru na kuokoa muda,"alisema Jaji Mzuna.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Arusha,John Mongella alisema kwa kuwepo miundombinu hiyo  inaonyesha dhamira ya dhati ya serikali kwa kushirikiana na mahakama kuboresha mifumo ya utoaji haki.

" Kama uongozi wa serikali ya mkoa tuwaahidi mahakama tutaendelea kuwapa ushirikiano wakati wote nadhani mnahitaji ushirikiano wetu  na mwisho wa siku uhimarishaji wa sekta hii ya mahakama vilevile utadhihirisha ubora wa mifumo yao ya  kiutawala na hasa dhana ya utawala bora,"alisema Mongella.

Mongella alisema uwekezaji, biashara  na yote yanayosimamiwa na serikali bila kuwa na mifumo mizuri ya sheria inawezekana isiwe na mvuto sana lakini wanafahamu uborehaji wa mifumo hiyo itaendana na utoaji wa haki vizuri na ufanisi kuliko ilivyo kuwa hapo awali.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI