Header Ads Widget

WAZIRI LUKUVI AWASHUKIA TENA MADALALI KUWA LAZIMA WALIPE KODI

 

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi William Lukuvi amesema sifa ya Dalali sio tu kujua kusoma na kuandika bali lazima wawe na Ofisi na walipe kodi ya Serikali.

“Dalali akikuomba kodi ya mwezi mmoja mwambie akupe risiti ya EFD kama anayo, na sifa za Madalalo sio tu kujua kusoma na kuandika hapana, lazima wawe na ofisi na walipe kodi kwa sababu wanafanya transactions za Mamilioni, Dalali anauza hadi nyumba ya Bilioni moja halafu halipi kodi”——— Waziri Lukuvi

Itakumbukwa juzi Waziri Lukuvi akiwa Iringa leo aliwapiga pia marufuku Madalali wa nyumba wanaochukua kodi ya mwezi mmoja kwa Wapangaji na kuwataka waache mara moja na badala yake pesa hizo walipwe na wenye nyumba

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI