Vyombo vya habari vya serikali ya Uturuki vimeripoti kuwa Handal anashikiliwa mjini Istanbul baada ya maafisa wa mahakama kutoa amri ya kuwekwa ndani kwa siku 40, kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press.
Handal ambaye ametajwa kama raia wa Haiti na vyombo kadhaa vya habari, alikamatwa baada ya kutua na ndege mjini Istanbul wakati wa kubadili ndege akitokea Marekani kuelekea Jordan.
Joseph alitweet kwamba alizungumza kwa njia ya simu na mwenzake wa Uturuki Mevlut Cavusoglu Jumatatu usiku baada ya Handal kukamatwa. Joseph hakutoa maelezo zaidi kuhusu iwapo Haiti itaomba arejeshwe nchini.
Kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kumetokana na juhudi za ulimwengu za kuwasaka wauaji wa Rais Jovenel Moise wakati alipokuwa akikumbana na hali ya ukosefu wa uthabiti wa kisiasa, uhaba wa mafuta, ghasia za magenge na njaa mbavyo vilifanya hali kuwa mbaya zaidi kutokana na tetemeko la ardhi la mwezi Agosti.
Chanzo; VOA Swahili





0 Comments