Header Ads Widget

WATUMIAJI WA MITANDAO YA KIJAMII WAONYWA

 


WATANZANIA wametakiwa kuacha kutumia vibaya mitandao ya kijamii kukashifu viongozi wa dini na waserikali badala yake waitumie kwa kujifunza na kujiletea maendeleo.

Rai hiyo imetolewa na   Balozi ambae  mratibu wa Bakwata Online Academy kanda maalumu inayojumuisha Mikoa ya Pwani, Arusha,Tanga na Kilimanjaro Alhaji Abdul Sharifu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuteuliwa kwenye nafasi hizo.

Sharifu alisema kuwa serikali ilitoa waraka Aprili mwaka 2020 kwa taasisi za dini kuhakikisha zinawapatia mafunzo viongozi wake ili wawe na ujuzi, maarifa na weledi wakati wa kutoa huduma kwa waumini na jamii.


Sharifu ambaye pia ni mwenyekiti wa Bakwata na CCM Wilaya ya Bagamoyo baada ya masomo hayo ya mtandao na kujiongezea ujuzi Mufti anawapatia vyeti wahitimu wanakuwa na uwezo wa kusomesha na kusimamia waumini wao.


Akizungumzia kuhusu utumiaji mbaya wa Tehama alisema baadhi wanatumia vibaya kukashifu viongozi wa dini na serikali ila Watanzania watumie mitandao kwa faida siyo hasara na kupata mafanikio kwa kutoa elimu mbalimbali kwa kuelimisha hata changamoto zilizopo.


Aidha alisema kuwa watu wanatumia vibaya kwa kubeza au kutukana wanapaswa kueleza mambo mazuri ya nchi mfano Rais kafanya mambo mazuri ya maendeleo watumie kutangaza mambo hayo ili watu waijue serikali yao na mambo yaliyofanyika katika nchi.


Kwa upande wake katibu wa Taasisi ya Shakiba Islamic Foundation Hassan Kilemba alisema wanampongeza mufti kwa kumteua kuwa Balozi na mratibu kanda maalumu ya Bakwata Online Academy  kwani hiyo itasaidia kuleta maendeleo kwa kanda maalumu ambayo ataisimamia.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI