Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Ngolo Malenya amewataka wajasiliamali kuchangamkia fursa ya kukopa pesa zinazotolewa na Halmashauri ili kukuza biashara zao na kupata maendeleo. mwandishi wa matukio daima Jacob Sonyo anaripoti kutokea Ulanga
Akizungumza katika kuelekea miaka 60 ya Uhuru, Malenya alisema serikali inataka kuwapa unafuu wajasiliamali na ndio maana mikopo hiyo kwa sasa inatolewa kwa kila mjasiliamali hivyo alisema ni vema wajasiliamali wachangamkie fursa hiyo.
Katika kuelekea miaka 60 ya Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Ngolo Malenya alipata nafasi ya kuona maenesho ya biashara zinazofanyika Wilayani Ulanga na kuzungumza na wajasilamali wanaofanya biashara wilayani ulanga.
Naye Afisa Maendeleo ya jamii Wilayani Ulanga Mohamed Atik ,alisema mikopo inatolewa kwa vijana, akina mama na walemavu kwa kufuata taratibu zilizowekwa ikiwemo ya kurejesha mikopo hiyo kwa wakati ili wengine wapate fursa ya kukopa.
0 Comments