Matukio Daima, Mombo
MASHABIKI na wapenzi wa klabu ya Soka ya Simba Mombo wilayani Korogwe Mkoani Tanga wanatarajia kufanya uzinduzi mkubwa wa tawi lake jipya mnamo Januari mosi 2026, katika viwanja vya Misajini, Jitengeni ikiwa ni sehemu ya mkakati wa klabu hiyo kuimarisha mtandao wa wanachama na mashabiki nchini.
Uzinduzi huo utaongozwa na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Mheshimiwa Mwita Mwazalendo maarufu kama Wakili Mwaza, huku mgeni mwalikwa wa heshina akiwa ni Mzee Hassan Dalali sambamba na viongozi wa juu wa klabu ya Soka ya Simba SC pamoja na viongozi wa matawi mbalimbali ya klabu hiyo.
Kwa mujibu wa ratiba, hafla hiyo itaanza majira ya saa 10:00 alfajiri kwa maandamano ya hamasa ya mashabiki yatakayopitia katikati ya mji wa Mombo kuelekea eneo la tukio kabla ya kufanyika kwa sherehe za utoaji wa hotuba, uzinduzi rasmi pamoja na hamasa ya uanachama kupitia mfumo wa kidijitali wa Simba App.
Madhumuni ya uzinduzi huo ni pamoja na kuimarisha umoja wa mashabiki, kuongeza wanachama wapya, kuchangisha fedha za uendeshaji wa tawi na kuleta nguvu mpya ya ushiriki wa mashabiki katika maendeleo ya klabu hiyo.
Hafla hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa michezo, mashabiki, wapenzi wa Simba kutoka maeneo mbalimbali ya Tanga na mikoa jirani






0 Comments