Ukaguzi wa ujenzi vyumba vya madarasa na Nyumba za walimu
Ukaguzi hatua Kwa hatua kuona ubora
VIONGOZI wa Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM)wilaya ya Tarime Vijijini mkoani Mara wakiongozwa na mwenyekiti wao na katibu wamefanya ziara ya kukagua miradi mbali mbali ya kimaendeleo inayotekelezwa na Serikali .
Viongozo hao wametembelea miradi hiyo ya ujenzi ikiwemo ya ujenzi wa vyumba vyaadarasa na vyumba za walimu na kufurahishwa na jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali pamoja na mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Mwita Waitara ambae ni Naibu Waziri wa ujenzi na uchukuzi .
UVCCM wilaya ya Tarime Vijijini wamempongeza mbunge wa Jimbo hilo Viongozi wa Halmashauri na mkuu wa wilaya Kwa ushirikiano wao Katia kutekeleza miradi ya kimaendeleo hasa ujenzi wa vyumba vya madarasa huku wakimshukuru Rais Samia Suluhu Samia Kwa uongozi uliotukuka na kuendelea kutoa fedha za miradi mbali mbali .
0 Comments