Header Ads Widget

MBUNGE ZUENA BUSHIRI ALIA NA WATU WENYE ULEMAVU NA WAZEE.




Na WILLIUM PAUL, MWANGA. 


KATIKA kuelekea Sensa ya watu na makazi mwakani wananchi wameshauri kutowaficha watu wenye ulemavu pamoja na wazee kwani nao ni haki yao kuhesabiwa ili kuweza kupata huduma ya mahitaji muhimu toka serikalini.



Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa viti maalum kupitia mkoani wa Kilimanjaro,  Zuena Bushiri wakati akizungumza na wanachama wa Umoja wa Wakinamama wa CCM (UWT)  tawi la Lembeni wilayani Mwanga.



Zuena alisema kuwa, lengo la serikali kufanya Sensa ni kujua idadi ya wananchi ili iweze kutoa huduma inayoendana na idadi ya wananchi iliyopo. 



"Watu wenye ulemavu pamoja na wazee nao zipo huduma ambazo ni haki yao kuudumiwa na serikali na ili kuhakikisha wanapata huduma hizo ipo haja ya kufanyiwa sensa nao ili kujulikana idadi yao" alisema Zuena. 



Akizungumzia swala la uchaguzi ndani ya chama mwakani, Mbunge huyo aliwataka wakinamama kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali ndani ya chama na jumuiya zake.



"Rais Samia Suluhu ambaye ni Mwenyekiti wa chama chetu amekuwa akisema waziwazi swala la asilimia hamsini kwa hamsini na sisi tunapaswa kumuunga mkono kwa kuwania nafasi mbalimbali na tuachane na tabia ya kukatishana tamaa" alisema Zuena. 


Aidha Mbunge huyo alisema kuwa serikali ya awamu ya sita itaendelea na kazi kubwa za kuhakikisha inaendelea kuboresha huduma za afya na kudai kuwa changamoto zilizopo katika zahanati ya kijiji cha lembeni zitapatiwa ufumbuzi. 





Awali akisoma risala kwa Mbunge huyo, Katibu wa UWT kata ya Lembeni, Mwanaharusi Hussein alisema kuwa,  zahanati ya Lembeni inayotarajiwa kuanza kazi wakati wowote inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa jiko maalum la kuchomea taka pamoja na kondo la nyuma kwa mama watakaojifungulia katika zahanati hiyo. 





Katika ziara ya Mbunge huyo mbali na kuzungumza na wanachama wa CCM pia alichangia matofali kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UWT wilaya. 







Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI