Mkuu wa koa wa Arusha John Mongela kuwa amesema kuwa vijana wanajukumu na wajibu mkubwa wa kuendeleza misingi ya usalama na amani ya nchi iliyowekwa na waasisi wa nchi ili misingi hiyo iweze kuendana na maendeleo makubwa yaliyopo hivi sasa ikiwemo masuala ya teknolojia.MWANDISHI NAMNYAK KIVUYO,MDTV ARUSHA
Mongela aliyasema hayo wakati akifungua kongamano la maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania bara iliyoandaliwa na chuo cha uhasibu Arusha (IAA) ambapo alisema kuwa ili kuenzi misingi hiyo ni vema kuiga mambo yaliyofanya na wazee katika kupigania uhuru lakini kwa njia ya kisasa.
“Wakati uhuru unapatikana jinsi ya kupata upeo wa mawazo ilikuwa ni ngumu lakini kwa sasa teknolojia imekuwa kwa kasi na kwa sekunde moja tu unaweza kujua kila kitu kinachoendelea Duniani kote kutokana na maendeleo makubwa yaliyopo katika teknolojia ya habari na mawasiliano,” Alisema Mongela.
Alifafanua kuwa kuna mambo mengi ambayo ni mafanikio ya miaka 60 ya Uhuru ikiwemo vyou kufundishia kwa njia ya mtandao na hasa chuo cha uhasibu ambapo kama vijana wanatakiwa kuangalia ni nini cha kufanya ili kiwe na mchangao kwa nchi katika suala la maendeleo.
“Ajenda ya kuijenga nchi ndio jambo tunalojivunia hadi sasa na ajenda hii ilitoka kwa hayati Mwalimu Julias Nyerere ambapo na chuo hiki Cha IAA ni chuo kinachifanya mtengemano wa kitaifa unaoendana na mustakabali wa nchi hivyo na ninyi vijana mnatakiwa kulenga mnachokitaka,”Alisema.
Alieleza kuwa ni vema vijana wakajituma na wakawa na malengo lakini pia kutokuwa na haraka ya kupitiliza itayowaingiza kwenye mambo yasiyofaa ambapo anaamini kongamano hilo litazaa tija kwa mkoa na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha (IAA) Profesa Eliamani Sedoyeka alisema kuwa chuo hicho kimepewa jukumu na serikali ya kuandaaa kongamano hilo ambapo kama chuo wameanzisha kitivo cha utalii na wakaona ni vema kongamano hilo likabeba mada uwekezaji katika utalii baada ya miaka 60 ya Uhuru.
“Taifa linajivunia mchango mkubwa wa maendeleo ulioletwa na sekta ya utalii kanda ya Kaskazini ambayo kwa kiasi kikubwa imeshikwa na watu binafsi,” Alisema Profesa Sedoyeka.
0 Comments