Jumla ya shilingi 97,520,000. zimepatikana kwenye mnada wa kwanza kwa kuuzwa jumla ya tani 46 za korosho ambazo zimetoka wilaya za ulanga na malinyi mkoani morogoro. mwandishi wa matukio daima Jacob Sonyo anaripoti kutokea Morogoro
Hayo yalisemwa na afisa ushirika halmashauri ya wilaya ya Ulanga Ester Mgaya, wakati wa kufanyika zoezi hilo la mnada ambapo alisema jumla ya tani 46 sawa na kilo 46,000/= zilipelekwa kwenye mnada huo ambao ndio mara ya kwanza kufanyika wilayani Ulanga ikishirikisha na Wilaya ya Malinyi.
Ester alisema kuwa wakulima wa wilaya hizi wanatakiwa kuwa na hali zaidi ya kulima zao hilo la Korosho kwani limeonekana kufanya vizuri katika wilaya hizi mbili Ulanga na Malinyi na kuachana na mazoea ya kilimo cha aina aina moja tu
Naye Afisa ubora wa zao la korosho Ahmad Salum aliwataka wakulima kufuata maelekezo ya uandaaji wa korosho kwa kuzitenganisha zenye ubora ambazo ndizo zinazo takiwa kupelekwa sokono ili kuondoa usumbufu mara wanapofika sokoni hapo.
Aidha wakulima wa korosho Wilayani Ulanga na Malinyi waliishukuru Serikali kwa kuweza kuwapelekea mnada huo karibu nao ,ambapo umeweza kurahisisha juu ya uuzaji wa korosho zao na wamewaomba Viongozi waweze kuwahimiza wanunuaji wa korosho kuwapelekea fedha za malipo wa wakati.
0 Comments