Header Ads Widget

JELA MIAKA 30 KWA KUIBA NA KULAWITI

Mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya nzega mkoani Tabora imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela mkazi wa Kijiji cha wita kata ya ndala mkoani hapa Maganga Antoni (30) baada ya kupatikana na mkosa mawili ya unyang'anyi kwa kutumia silaha na ulawiti. mwandishi wa matukio daima Lucas Raphael anaripoti kutokea Tabora

 

Akisoma hukumu hiyo hakimu mkazi wa wilaya ya nzega Mhere Mwita alisema kutokana na ushahidi usioacha Shaka uliotolewa mahakamani hapo mahakama hiyo imeridhia kumhukumu kifungo cha miaka 30 jela

 

Alisema ushahidi uliotolewa mahakamani hapo mahakama hiyo imeridhia adhabu hiyo ya kifungo cha miaka 30 jela na kuongeza kuwa adhabu hiyo iwe fundisho kwa watu wengine kwenye nia kama hiyo.

 

Kabla ya kusomwa kwa hukumu hiyo hakimu Mhere Mwita alielezwa na wakili wa serikali Jenipher Mandago aliiambia mahakama hiyo kuwa mnamo mwezi wa sita ya Tarehe 5 mwaka huu 2021 majira ya usiku huko katika Kijiji cha Ntoba kata ya Ndala wilaya ya nzega na mkoa huu wa Tabora Maganga Antoni alivamia nyumba ya mwanamke mmoja jina limeifadhiwa mkazi wa Kijiji hicho na kuiba kiasi cha  42,000/ na kisha kumbaka mwanamke huyo kwa kumlawiti.

 

Wakili huyo wa serikali aliongeza kwa kusema kutokana na kitendo hicho cha kinyama alichokifanya aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwake na kwa watu wengine.

 

Hata hivyo hakimu wilaya ya nzega alitoa nafasi ya utetezi kwa Maganga Antoni kabla ya kutiwa hatiani  aliomba kupunguziwa adhabu kutokana na kuwa na umri mdogo na familia inayomtegemea .

 

Mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya nzega haikuridhia na utetezi huo na ikamuhukumu Maganga Antoni kutumikia kifungo hicho cha miaka 30 jela ambapo atakitumikia kifungo hicho kwa wakati mmoja.







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI